HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 10, 2020

Mwakinyo atamba kumchapa Paz kwa KO, mabondia watambulishwa

 

  Bondia Hassan Mwakinyo na Muargentina Jose Carlos Paz wametamba kila mmoja atamchapa mwenzake katika pambano la kuwania ubingwa wa uzito wa super-welter wa mabara unaotambuliwa na chama cha WBF.

Mwakinyo na Paz watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Next Door Arena katika pambano lililopangwa kuwa la raundi 12.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Mwakinyo alisema kuwa atahakikisha Paz anaachana na mchezo wa ngumi za kulipwa kutokanana kipigo alichumuandalia.

“Natamani pambano lifanyike mapema iwezekanavyo, hata siku moja kabla kwani nipo fiti zaidi ya nilivyokuwa mwanzoni. Sitaki kuwanyong’onyesha Watanzania katika pambano hilo,” alisema Mwakinyo.

Alisema kuwa anajua kuwa Paz ni bondia mzuri na amejiandaa vyema katika pambano hilo, lakini kutokana na jinsi alivyojiandaa, hatakuwa na nafasi ya kutamba kwake.

Kwa upande wake, Paz alisema kuwa hakuja nchini kutembea zaidi ya kuwania ubingwa wa ambao Mwakinyo anao.

“Nipo vizuri, mazoezi yangu nchini yamekuwa na mafanikio makubwa na hali ya hewa siyo tatizo. Nitamfundisha ngumi Mwakinyo ,” alisema Paz.

Kwa mabondia hao kutambiana pia bondia Hussein Itaba na mpinzani wake kutoka DR Congo, Alex Kabangu, Fatuma Zarika dhidi ya Patience Mastara (Zimbabwe) na Mtanzania Zulfa Macho ambaye atazichapa na Alice Mbewe wa  Zambia pia walitambiana.

Mkurugenzi wa Jackson Group Sports, Kelvin Twissa alisema kuwa maandalizi yamekamilika na kuwaomba mashabiki kuendelea kununua tiketi kwa ajili ya pambano hilo.

“Maandalizi yapo vizuri na kama mnavyoona mabondia wote wapo hapa na sas tunamsubiri Rais wa WBF, Howard Goldberg na mwamuzi Edward John Marshall ambao watawasili leo Jumatano Novemba 11,” alisema Twisa.

Twissa alisema tiketi zitaanza kuuzwa kwa njia ya Nilipe na Selcom kwa Sh 3 Milioni kwa meza ya watu 10 na Sh150,000 kwa kwa viti vya kawaida. 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twissa akiwatambulisha Hassan Mwakinyo na Jose Carlos Paz ambao watawania mkanda wa mabara wa chama cha WBF wa uzito wa super-welter.  

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twissa akiwatambulisha Hussein Itaba wa Tanzania (kulia) na Alex Kabangu wa DR Congo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twissa akiwatambulisha Alice Mbewe wa Zambia (kulia) na Zulfa Macho wa Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twissa akiwatambulisha Fatuma Zarika wa Kenya na Patience Mastara wa Zimbabwe .



Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jackson Group Sports Kelvin Twissa akizungumza wakati wa utambulisho wa mabondia ambao watashiriki katika mapambano ya Jackson Group Fight Night yaliyopangwa kufanyika Novemba 13 kwenye ukumbi wa Next door Arena.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad