Karibu wa CCM Wilaya ya Longido Joseph Olesadira
Mogombea ubunge kwa tiketi ya CCM akizungumza na wananchi wa kata ya Longido Mjini na ile ya  orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika  Longido
Mwenyekiti
 wa CCM wilaya ya Longodo Joseph Olesadira akizungumza na wananchi wa 
Jimbo la Longido katika mkutano wa hadhara u;liofanyika jana na 
kushirikisha kata mbili ya Longodo
Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Ezekilel akizungumza na wananchi wa kata ya Longido Mjini na ile ya  orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika  Longido
Wananchi wa kata ya
 Longido Mjini na ile ya  orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika 
 Longido wakisikiliza sera za wagombea ubunge na udiwani katika jimbo 
hiloWananchi wa kata ya
 Longido Mjini na ile ya  orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika 
 Longido wakisikiliza sera za wagombea ubunge na udiwani katika jimbo 
hiloMgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Longido  Dkt.Stephen Kiruswa
 amesema kuwa atakapochaguliwa katika Jimbo hilo kwa kushirikiana na 
madiwani watahakikisha wanasimamia wazawa wanapata haki ya kumiliki 
Ardhi, bila kuwasahau wanawake na kupata stahiki zao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliyoandaliwa na Chama hicho kwa kata mbili za Longido mjini na Orbomba ,Kiruswa
 alisema kazi ya kutafuta Viongozi siyo kazi rahisi bali ni jambo gumu 
linalohitaji utayari kwaajili ya kuwatumia wananchi bila ubaguzi na 
kutatua changamoto zao ambapo yeye amesema yupo tayari .
Dkt.Kiruswa
 alisema kwamba kwa kushirikiana na madiwani katika Jimbo hilo mara 
baada ya Uchaguzi watahakikisha wanasimamia vyema maslahi ya wanalongido
 Ikiwemo miradi ya Afya,Maji ,Umeme,Elimu Ili kila mwananchi afaidike na
 miradi hiyo.
Wakizungumza wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Longido wakusema kuwa Dkt.John Pombe Magufuli
 amekuwa mzazi wa watoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari kwa
 kuwapatia Elimu bure bila malipo na kusababisha watoto wao kung'ara 
kielimu 
Sambamba na hayo Kamati hiyo ulisema kuwa wamekuwa wanufaika wakubwa wa maji ya mto Simba kuwafikia Longido, ikiwa ni juhudi za Magufuli na kuepuka adha ya kwenda kutafuta maji nchi jirani ya Kenya kwenye visima,kwa Sasa wanatumia maji Safi na salama. 
Akizungumzia changamoto iliyokuwepo awali ya Morani kujiandikisha na kuacha kupiga kura Diwani mteule kata ya Longido Thomas Ngobei 
alisema kuwa tayari wameshaweka utaratibu nzuri wa zamu ya kwenda 
machungani kwa awamu ili wengine wapate nafasi ya kupiga kura kama haki 
yao ya msingi
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Longido Ezekiel Mollel alisema
 kichama wana kata 18  hivyo  ujio wa mgombea Urais Taifa Dkt.Magufuli 
Mkoani Arusha, alisema (w) hiyo wamejipanga ipasavyo kumpokea kwa 
kishindo
Aidha
 alimalizia kwa kuwataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi siku ya 
tarehe 28/10/2020 kwaajili ya kumpigia kura Rais ,Wabunge na Madiwani wa
 chama cha mapinduzi kwani wananchi wenyewe wamejionea kwa macho 
maendeleo katika wilaya hiyo na kwa Taifa kwa ujumla.








No comments:
Post a Comment