Patashika Nguo Kuchanika Ndani ya Anfield Jumatatu Usiku - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 26, 2020

Patashika Nguo Kuchanika Ndani ya Anfield Jumatatu Usiku

 Mzunguko wa 3 wa EPL, Liverpool kuwakaribisha Arsenal.

MSIMU mpya wa Premier League umeanza vizuri sana! Baada ya mtanange wa kukata na shoka kuchezwa wikiendi iliyopita, wikiendi hii tunaendelea kunogesha EPL kwa mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal. Anfield patachimbika jumatatu saa 4 usiku.


Je, David Luiz ataweza kumzuia Mohamed Salah? Vipi kuhusu Aubameyang na Lacazatte, wataweza kuisumbua safu ya ulinzi ya Liverpool?

Majibu ya maswali haya yanavutia, ukizingatia “The Gunners” wameuanza msimu vizuri zaidi japokuwa timu zote zimeshinda michezo yao miwili ya mwanzo. Arsenal anafaida ya magoli akiwa na tofauti ya magoli 4 ukilinganisha na Liverpool wenye magoli 3.


Amini usiamini, wataalamu wa Meridian wameuthamini ushindi wa Arsenal kwa odds ya 6.07. Kama unawaamini vijana wa Arteta, kazi kwako kuwapa ticketi ya ushindi na ujipatie faida kubwa mfukoni mwako!

Mabingwa – Liverpool wamethaminiwa ushindi kwa odds ya 1.52.  Wakati matokeo ya sare yamethaminiwa kwa odds ya 4.21.


Wataalamu wa Meridian wamekuwekea ofa ya machaguo zaidi ya 1,200 ambayo unaweza kuyaangalia hapa.


Liverpool walibeba ubingwa msimu ulipita baada ya kupambana kwa miaka 30, hakika Jurgen Klopp anakila sababu ya kuendelea kufurahia mafanikio haya.


Upande wa pili, Arsenal tunaweza kusema walifeli msimu uliopita kwenye Premier League. “The Gunners” walimaliza katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa EPL. Japokuwa, vijana wa Arteta hawakutoka patupu msimu mzima, walibeba Kombe la FA na kuwapa tiketi ya kucheza Europa League msimu huu.


Mchezo kati ya Liverpool vs Arsenal unakuwaga ni burudani tupu. Unafahamu kama hii sio mara ya kwanza timu hizi kukutana msimu huu?

Arsenal wameshapeleka kilio kwa Liverpool msimu huu baada ya kuwagaragaza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii!


Tusubiri tuone kama Arsenal wataweza kurudia/. walichokifanya kwenye ufunguzi wa msimu mpya wa EPL, au kama Liverpool atalipa kisasi? 


Meridian - Nyumba yenye odds bora na bonasi kubwa!

18 comments:

Post Bottom Ad