KITUO CHA BIASHARA ZINAZOCHIPUKIA KUFANYA TAMASHA KUBWA LA UBUNIFU NA UVUMBUZI JIJINI ARUSHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 26, 2020

KITUO CHA BIASHARA ZINAZOCHIPUKIA KUFANYA TAMASHA KUBWA LA UBUNIFU NA UVUMBUZI JIJINI ARUSHA

 

Na Pamela Mollel,Arusha


Kituo cha Biashara zinazo chipukia (IAA Business Start Up Centre) kilichopo Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kinatarajia kufanya Tamasha kubwa la ubunifu na uvumbuzi liitwalo Arusha Innovation Summit mwezi November mwaka huu. 


Tamasha hilo linalo walenga wadau wa ubunifu na uvumbuzi litatoa nafasi ya mijadala mbali mbali yenye lengo la kukuza ubunifu na uvumbuzi nchini.


 Pamoja na mijadala, Tamasha hilo litakuwa kilele cha mashindano ya uvumbuzi na ubunifu yaitwayo Arusha Innovation Challenge yanayo shindanisha vijana mbalimbali toka nchini Tanzania waliofanya ubunifu na uvumbuzi wa vitu mbali mbali. 


Akizungumza na vyombo vya habari Jana katika chuo hicho cha uhasibu, msimamizi wa kituo hicho Bi Pamela Chogo amesema, mchakato wa vijana kushiriki kwenye mashindano ulianza jana tarehe 24 September kwa kuwawezesha vijana wanaopenda kushiriki kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tuvuti ya www.startup.iaa.ac.tz.


Alifafanua kwamba utaratibu wa jinsi ya kushiriki umeelezewa kwa undani kupitia tuvuti hiyo.


Bi Pamela aliendelea kusema kwamba kupitia Tamasha na shindano hilo, wanaendelea kuhamasisha vijana kujiajiri kupitia ubunifu na ugunduzi wanaoweza kuufanya.


Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo Sunday Massawe amesema kuwa washiriki wanaopaswa kushiriki mashindano hayo ni vijana kuanzia miaka 16 hadi 30 ambapo itawarahisishia vijana wenye ubunifu kuonyesha vipaji vyao ili kuweza kutambulika na jamii


Amesema kuwa wameamua kuwashirikisha vijana wote Tanzania walio vyuoni na walio nje ya vyuo na wa jinsi zote me na ke. 


Alisisitiza kwamba usajili umeshaanza na utafungwa oct 23 na baada ya usajili kutakuwa mchujo kwa hatua mbalimbali na mwisho kupatikana kwa mshindi. 


Mashindano hayo yamegawanyika katika makundi mawili ikiwa ni kundi la uvumbuzi kwenye tehama (ICT Innovations) na kundi la uvumbuzi kwenye kitu cha kijamii au kibiashara (Social and business Innovations )


Mwisho wa mchakato utatoa washindi watatu katika kila kundi ambao watapata zawadi.


Ndugu Sunday aliendelea kusisitiza kwamba mashindano ni ya vijana wotw na sio wasomi tu na wanawake wakipewa kipaombele.


Kwa upande wake mdau wa mashindano hayo ambayo ni Unisplash Bi Happy Mdenye amesema kuwa wamepata nafasi ya kuwa wadau ambapo watawafikia jamii kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii. 


Alisema wataendelea kutoa taarifa za kuweza kushiriki na kuwakumbusha vigezo na masharti, pamoja na kuendelea kutoa elimu mbalimbali


 Amewataka vijana kuwa na mazoe ya kutumia fursa zinazojitokeza ili kuweza kujifunza maswala mbalimbali ya kuwajenga katika Maisha.

 Msimamizi wa kituo cha Biashara zinazo chipukia kilichopo chuo Cha uhasibu Arusha Bi.Pamela Chogo katikati akizungumza na vyombo vya habari Jana  kuhusu Tamasha kubwa la ubunifu na uvumbuzi linalojulikana kwa jina la Arusha Innovation Summit litakalo lafinyika November mwaka huu,kulia ni mratibu wa mashindano hayo Sunday Massawe,kushoto ni mdau wa mashindano hayo kutoka Unisplash Happy Mdenye

 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiendelea na majukumu yao kwenye mkutano huo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad