Uongozi wa St.Mary's waahidi kuendelea kutoa elimu Bora - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 27, 2020

Uongozi wa St.Mary's waahidi kuendelea kutoa elimu Bora


Baadhi ya watarajiwa wahitimu wa Darasa la Saba Wavulana wakiwa katika mahafali ya 21 ya shule ya At.Mary's Mbagala jijini Dar es Salaam. 

Picha ya pamoja wakugenzi pamoja na walimu kwenye Mahafali ya 21 ya Darasa la Saba katika shule ya St.Mary's Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mtarajiwa Mhitimu wa Darasa la Saba Cleopatrarita Kato akizungumza kuhusiana na ndoto yake ya kuwa Daktari wa Watoto katika Mahafali ya 21 ya Darasa la saba shule ya St.Mary's Mbagala.
Mkuu wa Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu shule za St.Mary's Askofu Dkt.Getrude Rwakatare akiwasaa wazazi kuwapeleka wanafunzi katika shule hizo kutokana na utoaji wa elimu bora.
Baadhi ya watarajiwa wahitimu Wasichana wa Darasa la Saba wakiwa katika mahafali ya 21 ya shule ya At.Mary's Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya St.Mary's Mbagala Jacob Mwangi akizungumza kuhusiana na mahafali ya Darasa la saba yenye wahitimu 87 yaliyofanyika katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa St.Mary's Mutta Lwakatare akizungumza na watarajiwa wa wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya St.Mary's Mbagala jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
UONGOZI wa Shule za St.Mary's umesema kuwa utaendelea kusimamia shule hizo na kuendelea kushika rekodi nzuri katika matokeo licha kuondokewa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Askofu Dkt.Getrude Rwakatare.

Hayo aliyasema Mmoja wa Wakurugezi wa Shule hizo Mutta Rwakatare katika mahafali ya 21 ya Darasa la Saba Shule ya St.Mary's Mbagala amesema kuwa wamejipanga katika usimamizi na kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu bora itayowafanya vijana wanaohitimu kuwa tegemeo la Taifa.

Amesema kuwa watakwenda kisasa zaidi ikiwa ni pamoja ya kuwajenga watoto kimaadili ili wazazi waweze kunufaika na watoto wao kufikia ndoto wanazozitarajia katika elimu.

Nae Mkuu wa Shule hiyo Jacob Mwangi amesema kuwa katika matokeo ya Darasa la saba wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi kuliko matokeo ya mwaka jana.

Mwangi amesema kuwa shule bado iko katika ubora katika utoaji elimu kutokana na uongozi ulioachwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Dkt.Getrude Rwakatare.

Mhitimu Mtarajiwa Cleopatrarita Kato amesema kuwa walimu wamefundisha vizuri na kuahidi kufanya vizuri na ndoto yake ni kuwa Daktari wa Watoto kutokana na changamoto iliyopo ya Watoto.

Mwanafunzi wa shule hiyo Getrude Tende ambaye ni Mjukuu wa Askofu Getrude Rwakatare amesema Bibi ameacha shule katika mazuri na kutaka wazazi kuwa na imani ya shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad