HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 28, 2020

Mashabiki wa soka wawili washinda mamilioni ya M-BET

 Na Mwandishi wetu


Dar es Salaam. Mashabiki wa soka wawili nchini kila mmoja ameshinda kiasi cha Sh 79, 465, 240 baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.

Mashabiki hao ni Felix George Simba na Twalib Mfingile ambao wameshinda kupitia mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania.

Meneja masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa washindi hao wawili wameshinda jumla ya sh 159,930,480.

Mushi alisema kuwa kampuni yao itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwani washindi hao wawili ni wa tano tokea kuanza kwa msimu huu.

“Kama tulivyosema kuwa kushinda na M-Bet ni simple tuu na Mfingile na Simba wamedhihirisha kuwa kushinda na suala rahisi sana kutokana na aina ya mechi ambazo M-BET imekuwa ikizichagua kwa ajili ya mashabiki wa soka kubashiri,” alisema Mushi.

Alisema kuwa M-BET inajivunia kuwawezesha Watanzania kwa kubadilisha maisha yao ambapo mpaka sasa jumla ya washindi watano wamepatikana kupitia michezo yao ya kubashiri,” alisema Mushi.

Kwa upande wake, Mfingile alisema kuwa atatumia fedha hizo kwa kilimo cha kisasa na masuala mengine ya maendeleo katika familia yake.

“Mimi ni shabiki wa mpira lakini si kwa timu za Tanzania, napendelea zaidi timu za Ulaya na ndiyo nimeshinda kwa kutokana na kuzifuatilia kwa ukaribu sana,” alisema Mfingile ambaye ni mkazi wa Ifaraka, mkoani Morogoro.

Kwa upande wake, Simba alisema kuwa amejisikia faraja sana kubashiri na kushinda hasa kwa timu yake ya Arsenal ambayo inatamba sana kwenye ligi kuu ya England.

“Huwa Napata ugumu sana kutabiri mechi za Manchester United, hata hivyo nilifanikiwa kubashiri matokeo yake, Arsenal ni kushinda tu,” alisema Simba ambaye ni daktari mkoani Ruvuma.

Afisa Mamlaka Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, Shaaban Mwanga alisema kuwa malipo mashabiki hao watakatwa asilimia 20 kama kodi ya serikali.

Mwanga aliipongeza M-Bet kwa kuwa walipa kodi wa zuri nchini.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet, Allen Mushi (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi mfano wa hundi washindi wawili wa droo ya Perfect 12, Twalib Mfingile (wa pili kulia), Felix Simba (wa pili kushoto) ambao kila mmoja wamejishindia kiasi cha Sh 79,465,240. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa TRA kutoka mkoa wa Kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad