Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wajumbe wa Menejiment ya Wizara
hiyo leo Ihumwa jijini Dodoma wakati anawaaga kuanza ziara ya kutembelea
mradi ujenzi wa Reli ya ya Kisasa (SGR) ili kujionea maendeleo yake
ikizingatiwa Wizara hiyo ndiyo yenye dhamana kuisemea Serikali kupitia
Idara ya Habari (MAELEZO).


Wajumbe
wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa
katika wakitembelea handaki la nne eneo la Kilosa mkoani Morogoro
kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaojengwa
kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Mwanza.

Muonekano wa moja ya mahandaki itakapokuwa inapita Reli ya Kisasa (SGR) eneo la Kilosa Mkoani Morogoro.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM-Morogoro)
………………………………………………
Na Eleuteri Mangi, Morogoro
Ujenzi
wa Reli ya ya Kisasa (SGR) nchini unalenga kuleta maendeleo ya watu kwa
kurahisisha muda wa usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo ambapo
kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro itakuwa ni saa tatu au dakika 90
hatua itakayopunguza muda mwingi unaopotea barabarani na kuwafanya
wananchi kuwahi kufanyakazi nyingine za maendeleo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema hayo leo Ihumwa jijini Dodoma wakati
anawaaga Menejimenti ya Wizara hiyo kuanza ziara ya kutembelea mradi wa
SGR ili kujionea maendeleo yake ikizingatiwa hiyo ndiyo ni Wizara yenye
dhamana kuisemea Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).
“Wizara
ya Habari ni Wizara muhimu sana katika nchi yetu na mradi huu pia.
Ndiyo wizara yenye dhamana na habari kwa maana hiyo tumekuwa
tukiutangaza sana, na kuukiulinda mradi huu ili kuwaonesha watanzania
nini kinaendelea kwenye huu mradi” alisema Dkt. Abbasi.
Dkt.
Abbasi amesema kuwa Tanzania ipo makini kuwekeza kwenye mambo ambayo ni
muhimu katika kuleta manufaa na maendeleo ya watu na kusisitiza kuwa ni
utamaduni mpya kwenye nchi yetu kuwa na taifa la wachapakazi, kuwa
watanzania wanaojiamini na kuwa watu wanaopenda mambo mazuri ambayo
yanaletwa na Serikali kwa manufaa ya wananchi wake.
“Tunaposema
huu ujenzi wa reli ni kitu, ndiyo ni kitu, reli ya SGR ni kitu
kinachokwenda kuleta maendeleo ya watu. Utakapoweza kusafiri kwa saa
tatu au dakika 90 Dar es Salaam hadi Morogoro umepunguza muda mwingi wa
kupoteza barabarani na kuwahi kwenda kufanyakazi”alisisitiza Dkt.
Abbasi.
Mradi
huo ni moja miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali nchini na kuwa
miongoni mwa miradi mikubwa Afrika ambapo Serikali imewekeza trakriban
trilioni saba (07) kwa kipande cha Dar es Salaam, Morogoro hadi
Mkutupora mkoani Singida ambapo kipande cha Morogoro hadi Dodoma
kimefikia asilimia 42 hadi kukamilika kwake.
Akitoa
maelezo ya mradi huo kwa mwajumbe wa menejimenti ya wizara hiyo, Meneja
wa mradi kipande cha Morogoro hadi Mkakutupora mkoani Singida Mhandisi
Mteshi Tito amesema reli hiyo itatumiwa na treni ya abiria ambayo
itakuwa na mwendo wa kasi ya kilometa 160 kwa saa na ya mizigo itatumia
saa moja kwa kilometa 120 hatua inayopelekea mradi huo kuwekewa uzio
kuanzia mwanzo hadi mwisho ili kuepusha muingiliano wa watu wakati wa
kutekeleza majukumu yao.
Mhandisi
Mteshi ameongeza kuwa kipande cha reli ya SGR kati ya Morogoro na
Mkutupora Singida kina jumla ya km 422 ambapo km 336 zinajumuisha njia
kuu na km 86 sehemu za kupishania treni.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Menejiment ya Wizara
hiyo imeshuhudia na kujionea wenyewe uwekezaji mkubwa uliofanywa na
Serikali na kuongeza itakapokamilika reli hiyo kutakuwa na usafiri wa
uhakika kutoka Dar es Salaam hadi Mkutupora Singida ambayo itakuwa na
manufaa kiuchumi katika sekta ya usafirishaji.
No comments:
Post a Comment