HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 26, 2020

CHADEMA YAZINDUA RASMI KAMPENI ZA UBUNGE SONGEA

 

 Mgombea Ubunge wa jimbo la Songea mjini kwa tiketi ya Chadema Aden Mayalla wa pili kushoto akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama hicho mkoa wa Ruvuma na Kanda ya Mbeya wakiwa katika maandamano ya hiari mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya soko kuu mjini Songea jana. Picha  na Muhidin Amri

Na Muhidin Amri, Songea

MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Songea mjini kwa tiketi ya Chadema Aden Mayalla amesema,kukosekana kwa soko la uhakika la kuuzia mazao yanayozalishwa kwa wingi katika jimbo hilo kumetokana na kutowajibika kwa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana  ya kuwatumikia wananchi.

Hivyo, amewaomba wanachi wa jimbo  hilo wamchague  awe mbunge ili aweze  kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa soka la kuuzia mazao ya wakulima ambayo  sasa yanauzwa kwa bei ndogo licha ya gharama kubwa za uzalishaji.

Mayalla amesema hayo jana katika mkutano wake wa kampeni  uliofanyika viwanja vya soko kuu mjini Songea, na amewataka wananchi wa Songea kuhakikisha wanakipigia kura nyingi Chadema  ili kukiondoa  Chama cha Mapinduzi madarakani mabcho kwa muda mrefu kimeshindwa kuisimamia Serikali.

Mayalla amesema, endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo ataanza na utatuzi wa kero zinazowakabili wananchi wa Songea kwa muda mrefu hasa suala la soko la mazao,maji mindombinu ya barabara na kuondoa fedha ya malipo ya kadi ya mgonjwa kabla ya kuonana na Daktari.

Alisema, mkoa wa Ruvuma umebarikiwa kuwa na ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama korosho,kahawa,mahindi na ufuta, hata hivyo bado wananchi wake ni maskini ikilinganisha na mikoa mingine hapa nchini.

Aidha mgombea huyo amesema, iwapo atachaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anarudisha vyuo vyote vilivyofutwa na Serikali ya CCM ili kutoa fursa kwa watoto wa jimbo la Songea na mkoa wa Ruvuma kupata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu  ili nao waweze kufanya kazi za kuchangia maendeleo katika mkoa huo.

“nawaomba sana wananchi wenzangu wa  Songea mjini tarehe 28 Oktoba mnichague mimi Mayalla niwe mbunge wenu na Mheshimiwa Tundu Lissu katika nafasi ya Urais,Songea tumebaki nyuma kwa muda mrefu licha ya rasilimali nyingi  tulizonazo ikiwemo madin”alisema.

Mbali na changamoto ya soko la mazao Mayalla amesema, iwapo Chadema itachaguliwa na kushika dola itahakikisha inajenga upya barabara ya Njombe-Makambako  kwa kiwango cha lami kwani muda wake umekwisha jambo linalochangia ajali za mara kwa mara.

Kwa upande wake, kada wa Chadema kutoka mkoa wa Mbeya John Mwambigili amesema, wananchi wa jimbo la Songea wanakabiliwa na changamoto nyingi hali ilirudisha sana maendeleo na kutolea mfano kujengwa kwa kituo kipya cha mabasi eneo la Shule ya Tanga umbali wa km 30 kutoka mjini.

Kwa mujibu wa Mwambigili,Manispaa ya Songea haijawatendea haki wananchi kupeleka kituo hicho Shule ya Tanga kwani sio wote wenye uwezo wa kulipia usafiri kutoka mjini hadi  katika kituo hicho pale wanapohitaji kusafiri.

Kwa hiyo, amewaomba wananchi kutorudia makosa kwa kumchagua mbunge aliyemaiza muda wake Dkt Damas Ndumbaro  badala yake kuhakikisha wanamchagua Mgombea  ubunge wa Chadema Aden Mayalla ambaye ni msikivu na amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za kijamii na wananchi.

Alisema, haiwezekani na haingii akilini kuona mji wa Songea licha ukongwe wake umebaki kama kambi ya wakimbizi kwa kukosa  maendeleo  licha ya kuwa kituo kikuu cha kuuzia mazao na bidhaa mbalimbali na watu kutoka wilaya nyingine za mkoa wa Ruvuma  kama Mbinga,Namtumbo na Tunduru.

Naye mwanachama mkongwe wa Chadema Joseph Fume, amewaomba wakazi wa Songea kutorudia makosa ya kumrudisha tena Dkt Ndumbaro kwani katika kipindi chake cha miaka mitano hakuna maendeleo yaliyopatikana katika jimbo hilo.

Alisema,njia pekee ya kumuondoa madarakani ni kumnyima kura tarehe 28 Oktoba kwa kuwa ameshindwa kuliongoza jimbo hilo licha ya tabia yake kung’ang’ania nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad