NSSF YATEKELEZA MAAGIZO YA JPM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 17, 2020

NSSF YATEKELEZA MAAGIZO YA JPM

 

Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, imeridhishwa na utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kukamilishwa kwa ujenzi wa kipande cha barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni.


Jenista alisema hayo mwishoni mwa wiki, katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo hayo, ambapo alishuhudia ukamilishwaji wa ujenzi wa kipande hicho cha barabara ukiwa katika hatua za mwisho na unatarajiwa kukabidhiwa rasmi Agosti 31, mwaka huu.


Alisema ujenzi wa barabara hiyo unaenda vizuri na umefikia mwishoni, na kwamba mradi huo wa kihistoria ambao ni tegemeo kubwa kwa Watanzania hasa wakazi wa Kigamboni utakabidhiwa rasmi.


Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Balozi Ali Iddi Siwa, alimshukuru Waziri Jenista kwa namna anavyosimamia mambo yote yaliyo chini ya Wizara yake na kutoa miongozo.


Wakati huohuo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, alisema kukamilika kwa barabara hiyo ni manufaa kwa nssf kama kitega uchumi na manufaa kwa wakazi wa Kigamboni kwa sababu usafiri katika eneo hilo utakuwa nzuri zaidi na utafungua fursa nyingi za kiuchumi na kijamii.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akishuhudia mafundi wakiendelea na kazi ya usambazaji wa lami katika barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni, mwishoni mwa wiki.

 Mafundi wakiendelea na kazi ya kuweka lami katika barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni.

 Mwendesha Bodaboda, Godfrey Kurumwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, ambapo aliipongeza Serikali kwa kukamilisha mradi huo wa barabara.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista  Mhagama (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio (kushoto), alipotembelea nyumba za NSSF zilizopo Dungu, mwishoni mwa wiki.

 Mkazi wa Kigamboni, Meja Mstaafu wa JWTZ, Adiel Raphael Kaay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ubora wa barabara inayounganisha Daraja la Nyerere. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,  kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF Balozi Ali Iddi Siwa.

Mjasiriamali Mwajuma Salumu Shukuru akiishukuru Serikali na NSSF, kwa kukamilisha ujenzi wa kipande cha barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni, na kuainisha kuwa kabla ya barabara hiyo ya lami walikuwa wanapata shida  kubwa ya vumbi. Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad