Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara na mgeni
rasmi akizinduwa maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika
Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, Mkoani Dodoma leo yalioandaliwa na
Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET). Kulia Mratibu wa Taifa wa TENMET,
Bw. Ochola Wayoga.
Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga (kulia) akizungumza katika maadhimisho hayo.
Kutoka kushoto ni Afisa Elimu Sekondari Chemba, Valentine
Christopher na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara
wakiwa meza kuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara na mgeni
rasmi katika maadhimisho ya Juma la Elimu akipokea begi lenye mchapisho
ya maadhimisho hayo kutoka kwa Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola
Wayoga, alipotembelea banda la TENMENT kwenye maadhimisho hayo
yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, Mkoani Dodoma leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kulia)
akipata maelezo alipotembelea Banda la TENMET katika maadhimisho ya Juma
la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba,
mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kulia)
akipata maelezo alipotembelea Banda la TENMET katika maadhimisho ya Juma
la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba,
mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kulia)
akipata maelezo alipotembelea Banda la UWEZO katika maadhimisho ya Juma
la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani
Dodoma. Katikati ni Mratibu wa Uwezo Mkoa wa Dodoma, Nason Nason
akifuatilia,
Mratibu wa Uwezo Mkoa wa Dodoma, Nason Nason (katikati)
akimuonesha moja ya machapisho yao Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Mh. Mwita Waitara (kulia) alipotembelea Banda la UWEZO katika
maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya
Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kushoto)
akipokea maandamano kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika
katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara (kushoto)
akipokea maandamano kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika
katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Bendi ya matarumbeta ikiongoza msafara wa maandamano kwenye
maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya
Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu
yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi wakiwa na mabango ya jumbe mbalimbali
kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya
Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi wakiwa na mabango ya jumbe mbalimbali
kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya
Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika wilayani Chemba, mkoani Dodoma.
Maandamano ya wanafunzi kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu
yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara
alipotembelea Banda la Watoto Wetu Tunu Yetu-Dodoma katika maadhimisho
ya Juma la Elimu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi
Chemba, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara
alipotembelea Banda la HakiElimu katika maadhimisho ya Juma la Elimu
yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, mkoani Dodoma.
Na Joachim Mushi, Chemba
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mh. Mwita Waitara ameupongeza
Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa jitihada inazozifanya pamoja na
wanachama wake kwa kuiunga mkono Serikali hasa katika sekta ya elimu
kushirikiana tutatua baadhi ya changamoto za elimu.
Naibu Waziri Waitara ameyasema hayo leo wilayani Chemba alipokuwa
akizinduwa maadhimisho ya Juma la Elimu mwaka huu yanayofanyika katika
Viwanja vya Shule ya Msingi Chemba, ikiwa ni kuleta chachu ya
uwajibikaji kwenye sekt ya elimu kwa familia za wafugaji na jamii.
Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe
Magufuli ilipoingia madarakani ilibaini kuna kundi ambalo la watu
wasiojiweza walikosa elimu kutokana na changamoto mbalimbali za
uchangiaji, hivyo iliamua kuja na mfumo wa kutoa elimu bila ada.
"...Kulikuwa kuna watoto walishindwa kwenda shule, hivyo Rais John
Pombe Magufuli akaamua elimu kuanzia ya awali mpaka kidato cha nne iwe
bure, kwa maana kwamba elimu bila ada. Hii ndio inaitwa elimu msingi
bila malipo. Maamuzi hayo yalipata mafanikio makubwa kwani iliongeza
uandikishaji na ufaulu,"
"..Uandikishaji ulipanda kutoka watoto milioni 10 hadi milioni 12
hili ni jambo kubwa na tunampongeza mheshimiwa Rais Magufuli kwa kuliona
hilo, maana wapo vijana ambao walikuwa mtaani lakini sasa walienda
shule na kuendelea na masomo kidato cha nne hadi cha sita, na pia
wengine wameenda hadi vyuo," alisema Waitara na kuongez kuwa Serikali
inatumika takribani bilioni 24 kila mwaka kwa ajili ya kuwezesha mpango
huo wa serikali.
Aliongeza kuwa baadaye mwongozo ulitoka wa waraka namba tatu wa mwaka
2016 ulioonesha namna ambavyo jamii inashirikishwa kuchangia kutatua
changamoto ndogondogo kwenye elimu ili kuboresha zaidi.
Alisema Serikali licha ya kutoa elimu bila malipo haijafanikiwa kutoa
chakula kwa shule zote, hivyo imeelekeza wazazi wanaweza kujipanga na
kuchangia chakula ili mtoto aweze kujifunza huku akipata mlo jambo
ambalo linaweza hata kumfanya akaweza kushiriki kikamilifu kupokea
mafunzo toka kwa walimu.
Pamoja na hayo, alibainisha kumekuwa na wazazi ambao wamekuwa
hawaupokei vizuri mpango huo wa kuchangi na ndio maana yapo mashirika
yanajitolea kusaidia suala hilo, na hata nyie (TENMENT) nimeona
mkihamasisha wazazi kujitokeza kuchangia ili kupunguza changamoto katika
sekta hii. Lazima tuelewe kuwa hawa watoto ni wakwetu, shule ni za
kwetu na nijukumu la jamii kusaidia watoto wetu.
Aidha alisema jambo lingine ambalo linajitokeza kwa sasa ni wazazi
kujiweka pembeni kwenye ufuatiliaji taarifa za mtoto wake awapo shuleni,
wapo wazazi ambao wakishapeleka mtoto shule wao hujivua kabisa
kufuatilia taarifa za mtoto na mwishoni wanajitokeza kumlaumu mwalimu
pale mtoto anapofeli mtihani wa mwisho hili sio sawa wazazi lazima
tubadilike tufuatilie elimu ya watoto wetu.
Naye Mratibu wa Taifa wa TENMET, Bw. Ochola Wayoga alisema
maadhimisho ya mwaka huu yamelenga kuhamasisha uelewa wa jamii juu ya
haki ya kupata elimu, kuongeza uhamasishaji kwa jamii juu ya uwajibikaji
wa pamoja wa elimu na kuhamasisha Serikali kuzingatia na watoto wenye
uhitaji, ikiwemo miundombinu ya shule, vifaa vya mafunzo na mafunzo ya
ualimu.
Amebainisha kuwa kutokana na changamoto zilizopo katika sekta ya
elimu, Serikali haipaswi kuachiwa kila kitu hivyo wadau wanakila sababu
ya kujitokeza na kushiriki kuchangia masuala mbalimbali kwenye sekta
hiyo kusaidia kutatua baadhi ya changamoto.
Katika maadhimisho hayo yalioambatana na maonesho ya shughuli za
wanachama wa TENMET, yatashirikisha uchangiaji wa gharama za ujenzi wa
bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Kwamtoro iliyopo Wilaya ya
Chemba.
Maadhimisho hayo yanaofikia tamati Agosti 21 yataambatana na mijadala
mbalimbali, midahalo, ushiriki katika utoaji wa elimu kupitia vyombo
vya habari juu ya masuala anuai ya elimu na changamoto zake kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment