HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 10, 2020

TANESCO YAOKOA MABILIONI YA FEDHA MRADI WA UMEME TABORA-KATAVI

Na Mwandishi Wetu, Katavi 
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeokoa kiasi cha takribani Sh.bilioni 65 katika utekelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme mkubwa wa gridi ya Taifa kutoka mkoani Tabora mpaka Katavi wenye urefu wa kilomita 381. 

Mradi huo hapo awali ulikuwa ugharimu Sh.bilioni 135 lakini kwasasa utagharimu Sh.bilioni 70 ukijengwa na wataalamu wa TANESCO kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya TANESCO inayohusika na Ujenzi wa miundominu ya usafirishaji na usambazaji Umeme (ETDCO). 

Akikagua ujenzi wa Mradi huo, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameonesha kufurahishwa na jinsi ambavyo TANESCO imeonesha ubunifu uliopelekea kuokoa kiasi hicho kukubwa cha fedha ambacho kingetumika kumlipa mkandarasi kununua vifaa vya ujenzi wa nguzo za chuma toka nje ya mchi. 

Katika mradi huo, TANESCO wanajenga njia itakayosafirisha umeme wa kiwango kile kile ambacho kingesafirishwa katika nguzo za chuma lakini kwa kutumia nguzo za bei nafuu za miti zinazopatikana hapa nchini. 

"Nalipongeza Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa usimamizi mzuri, na niwatake kuendelea na usimamizi wa ujenzi wa line hii ya kusafirishia umeme na pia niwatake kuendelea kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa mradi huu ili ukamilike kwa haraka na ubora kama ilivyopangwa bila kuchelewa,"amesema Mgalu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad