MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM NEC UKUMBI WA WHITE HOUSE JIJINI DODOMA LEO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 10, 2020

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM NEC UKUMBI WA WHITE HOUSE JIJINI DODOMA LEO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC kilichofanyika katika ukumbi wa White House jijini Dodoma leo tarehe 10 Julai 2020.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula mara baada ya kuanza kikao cha NEC katika Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM NEC mara baada ya kuanza kwa Kikao ambacho kilikuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo ya Uchaguzi wa Mgombea wa Urais kwa upande wa Zanzibari ambapo Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi alichaguliwa kuwa kuwa Mgombe Urais kwa Tiketi ya CCM kwa upande wa Zanzibar leo tarehe 10 Julai 2020 katika Ukumbi wa White House jijini Dodoma 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kumpata mgombea Urais wa Zanzibar, uliofanyika katika jengo la Makao Makuu ya CCM White House Jijini Dodoma.(Picha na Ikulu) MGOMBEA  Urais wa Zanzibar Mhe. Hussein Ali Hassan Mwinyi akijieleza na kuomba kura kwa Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, uliofanyika katika ukumbi wa Makao Mkuu ya CCM  White House Jijini Dodoma , kumpata mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.(Picha na Ikulu) MGOMBEA  Urais wa Zanzibar Mhe.Shamsi  Vuai Nahodha akijieleza na kuomba kura kwa Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, uliofanyika katika ukumbi wa Makao Mkuu ya CCM  Whit House Jijini Dodoma , kumpata mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.(Picha na Ikulu) MGOMBEA  Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed , akijieleza na kuomba kura kwa Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, uliofanyika katika ukumbi wa Makao Mkuu ya CCM  Whit House Jijini Dodoma , kumpata mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.(Picha na Ikulu) WAGOMBEA Urais wa Zanzibar katika Chama cha Mapinduzi  waliopita Tano Bora na kupatikana Wagombea Watatu wakiwa katika ukumbi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli  akiongoza kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa  Makao Makuu ya  CCM Jijini Dodoma  White House, kumpa mgombea mmopja wa CCM kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.(Picha na Ikulu)WAJUMBE wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magifuli (hayupo pichani) akifungua Kikao hicho kilichofanbyika katika ukumbi wa  jengo la Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma White House, kumchagua Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.(Picha  na Ikulu)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi katika Mkutano huo wa NEC uliofanyika katika Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma.
 PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad