HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 20, 2020

Parimatch yaendelea kushika kasi ya ubunifu katika michezo ya kubashiri


Na, Mwandishi Wetu.
Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch mara baada ya kumaliza kufanya maboresho yake katika tovuti yao ya kubashiri na kuongeza michezo lukuki ikiwemo Casino, sasa imewageukia watumiaji wa simu za iphone (iOS) kwa kuwapa fursa ya kubashiri popote.

Kwa sasa watumiaji wa Parimatch  wanaweza kupakua App ya Parimatch  kutoka App store na kuendelea kufurahia msisimko wa kuvuna pesa.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Parimatch Tanzania,  Tumaini Maligana wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mfupi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kusema kwamba kwa sasa watumiaji wa simu za iphone (iOS) pamoja na zile za Android watapata kufurahia kupata kucheza na kushinda michezo yote mikali inayotolewa na Parimatch kwa kubonyeza https://pma.bet/parimatch


“Kutokana teknolojia kuwa na manufaa makubwa katika nyanja nyingi za kijamii hususani tasnia ya michezo ya kubahatisha, nasi tukaona itakuwa sio jambo la busara kama kuona kundi fulani la wateja wetu wanashindwa kupata huduma zetu bora kutokana na aina fulani ya simu zao wanazitumia," 

Pia, Maligana amesema, kuwa na App ya iOS ulikuwa ni mpango wao wa muda mrefu huko nyuma ila tunashukuru kuona tumeweza kuwafikia wateja wao wote kwa sasa.


Maligana ameendelea kwa kusema kuwa “kupitia tovuti yetu ya Parimatch pma.bet/parimatch wataweza kufurahia kucheza na kushinda michezo yote mikali pamoja na kupakua App mpya kwa watumiaji wa iOS na kujionea wenyewe raha ya burudani ilivyo kwa kubeti na Parimatch"

Pamoja na hayo, Maligana amedai kwamba Parimatch imejipanga vilivyo katika kulichangamsha soko la michezo ya kubahatisha kwa kutoa huduma bora zaidi pamoja na promosheni za kibabe kwa wateja wake wote waliopo kila upande wa nchi ya Tanzania.
Meneja Mkuu  wa Parimatch Tanzania,Tumaini Maligana akizungumza na waandishi wa habari.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad