HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 18, 2020

Dkt.Temu:Warithisheni Utamaduni Watoto na Vijana


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akipongeza Kikundi cha Utamaduni cha  Nyati Mchoya (hawapo pichani) kwa namna wanavyorithisha utamaduni kwa watato na vijana leo katika ziara ya kutoa elimu ya uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa utamaduni katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma. Kikundi cha Ngoma cha Nyati Mchoya kilichopo katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma kikicheza ngoma ya asili ya jamii ya Wagogo mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hayupo pichani) leo katika ziara ya kutoa elimu ya uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa utamaduni. Kikundi cha ngoma cha watoto cha kiitwacho Nyati C kikitoa burudani ya ngoma mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kutoa elimu ya uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa utamaduni iliyofanyika katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma. Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Msamaria kutoka Kijiji cha Nzali mara baada ya ziara ya kutoa elimu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Utamaduni iliyofanyika leo katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma.Kiongozi wa Kikundi cha Nyati Mchoya Bw. John Mchoya  akitoa ombi kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hayupo pichani) la kusaidia baadhi ya vikundi visivyo na uwezo wa kujisajili BASATA pamoja na kusaidia vikundi  vidogo kupata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali za serikali na matamasha katika ziara ya kutoa Elimu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Utamaduni iliyofanyika katika Kijiji cha Nzali,Kata ya Chilonwa, Dodoma.
********************************
Na Anitha Jonas – WHUSM, Chamwino
18/07/2020
Dodoma.
Wazee wa jamii za kitanzania wasisitizwa  kurithisha mambo ya utamaduni  kwa watoto na vijana ili tamaduni hizo ziweze kuendelea kwa vizazi vijavyo.
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu alipokuwa katika ziara kutoa Elimu ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Urithi wa Utamaduni alipotembelea kikundi cha Utamaduni cha Nyati Mchoya, kilichopo katika Kijiji cha Nzali, Kata ya Chilonwa, Dodoma.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwarithisha watoto na vijana shughuli za utamaduni hii inasaidia mambo haya kuendelea hata kwa vizazi vijavyo na msipofanya hivi mnahatarisha asili ya utamaduni wenu kupotea,”alisema Dkt.Temu.
Akiendeleza kuzungumza katika ziara hiyo Dkt. Temu alisema kuwa serikali inataka kupanua wigo wa utalii na kuifanya sekta ya Utamaduni kuwa ya utalii hivyo nijukumu la kila mtanzania kulinda na kuhifadhi utamaduni wake kwani nchi hii inautajiri mkubwa katika sekta hiyo ambao unaweza kukuza uchumi wa mwananchi kwa urahisi zaidi kutoka na namna ya uendeshaji wake.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo aliendelea kutoa wito kwa watanzania kuwa wanajitokeza kwenda kuangalia burudani  za utamaduni kama wanavyojitokeza kwenda kutazama mpira, na kusema serikali inatarajia kuanzisha matamasha mbalimbali ya utamaduni kwa lengo la kukuza na kutangaza utamaduni wa mtanzania.
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Maadili na Urithi wa Taifa Bw.Boniface Kadili alipongeza uongozi wa vikundi vilivyotoa burudani  ya ngoma kwa namna walivyonesha sanaa yao kwa kuzingatia kuzingatia uchezaji wa asili ambao hauna kuiga watu wa nje, zana za jadi walizotumia pamoja na uvaaji wa maleba.
Aidha, naye Kiongozi wa Kikundi cha Nyati Mchoya Bw. John Mchoya alitoa ombi kwa wizara la kusaidia baadhi ya vikundi visivyo na uwezo wa kujisajili BASATA pamoja na kusaidia vikundi hivyo vidogo kupata fursa za kushiriki shughuli mbalimbali ikiwemo matamasha na shughuli za serikali.
Halikadhalika nae mmoja wa kikundi cha Msamaria Bibi. Rhoda Petro alishukuru uongozi wa wizara kwa kuwatembelea na kuwa kutoa elimu ya namna ya kuhifadhi utamaduni wao na kuwaomba kurudi tena wakati mwingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad