HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 18, 2020

WAGOMBEA UBUNGE 283 SINGIDA WARUDISHA FOMU TAKUKURU YATOA ONYO WASIJIHUSISHE NA RUSHWA


Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu (kulia) akitoa taarifa jana kuhusu idadi ya wagombea ubunge wa chama hicho, Mkoa wa Singida waliorudisha fomu. Kusho ni Katibu wa UVCCM wa mkoa huo, George Silindu.
Afisa kutoka TAKUKURU Mkoani hapa, Samson Julius akitoa mada kwa wagombea hao.
Wagombea Ubunge wa chama hicho, Mkoa wa Singida wakiwa katika semina ya kutojihusisha na vitendo vya rushwa iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa.
Wagombea Ubunge wa chama hicho, Mkoa wa Singida wakiwa katika semina hiyo.

Wagombea Ubunge wa chama hicho, Mkoa wa Singida wakiwa katika semina hiyo.



Na Dotto Mwaibale, Singida.

WAGOMBEA nafasi ya Ubunge wa Majimbo na wa viti Maalumu 283 wamekwisha rudisha fomu za kuomba ridhaa ya kupitishwa kugombea nafasi hizo huku Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa ikitoa onyo kwa wagombea kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu akitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari alisema mkoa huo una jumla ya majimbo nane ambapo katika nafasi ya ubunge wa majimbo pekee ni wagombea 233, huku viti maalumu wakiwa 51.

Katika Jimbo la Singida mjini waliojitokeza kugombea nafasi ya ubunge ni 30 kati yao wanawake 2, Singida kaskazini ni 34 kati yao wanawake 3, Singida mashariki ni 10 na Jimbo la Singida magharibi ni 14.

Jimbo la Iramba magharibi waliojitokeza ni wagombea 30 kati yao wanawake 3, Iramba mashariki ni 51 kati yao wanawake 2, Manyoni mashariki ni 35 kati yao wanawake 4 na Manyoni magharibi ni wagombea 24.

Upande wa ubunge viti maalumu jumuiya za CCM,Uwt 44,Vijana 6 na upande wa jumuiya ya wazazi amejitokeza mgombea mmoja pekee.

Aidha kaburu alisema taratibu zote za uchaguzi zimeshakamilika ambapo uchaguzi kwa upande wa majimbo utafanyika July 20, UWT July 23, UVCCM July 30,na jumuiya ya wazazi ni July 31 mwaka huu.

Hata hivyo wagombea wote 30 wa ubunge wa jimbo la Singida mjini baada ya kukamilika zoezi la kurejesha fomu walipata fursa ya kukutana na Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa na kukumbushwa kufuata taratibu za uchaguzi.

Afisa kutoka TAKUKURU Mkoani hapa, Samson Julius akitoa mada kwa wagombea hao baada ya kurudisha fomu alitoa onyo kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kujikuta wanaingia kwenye mikono ya TAKUKURU.

"Zingatieni maadili kwa kufuata taratibu vinginevyo mtajikuta mpo mikononi mwa ( TAKUKURU) alisema Julius.

Alisema TAKUKURU haitaogopa kumchukulia hatua za kisheria mgombea yeyote atakaye kiuka maadili na kushindwa kufuata taratibu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad