HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 6 August 2019

BENKI CRDB YAENDELEA KUONGOZA KWA FAIDA SOKONI HUKU FAIDA YAKE IKONGEZEKA KWA ASILIMIA 98% KIPINDI CHA MWEZI JANUARI MPAKA JUNI 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitangaza faida ya TZS 86.65 bilioni  kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 ambayo ni ongezeko la asilimia  98%  kutoka  TZS 43.85 iliyoipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita  2018, katika mkutano uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts na Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo, Fredrick Nshakanabo. 

Benki  ya CRDB imetangaza faida ya TZS 86.65 bilioni  kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 ambayo ni ongezeko la asilimia  98%  kutoka  TZS 43.85 iliyoipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita  2018.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ongezeko la faida hiyo limetokana na kuimarika kwa mazingira ya biashara na jitihada binafsi za benki  na ongezeko pato litokanalo na biashara za fedha za kigeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitangaza faida ya TZS 86.65 bilioni  kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 ambayo ni ongezeko la asilimia  98%  kutoka  TZS 43.85 iliyoipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita  2018, katika mkutano uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
“Mwaka 2019 umekuwa na mafanikio kwa Benki ya CRDB. Mapato na faida yetu vimeongezeka kutokana na kuimarika kwa mapato halisi ya riba na mapato halisi yasiyo ya riba. Tulifanikiwa pia kuongeza kiwango cha mikopo huku tukishusha uwiano wa mikopo chechefu. Mikopo tuliyotoa kwa wateja iliongezeka sambamba na amana za wateja huku tukiwafikia wateja wapya kupitia huduma za kidijitali kama vile SimBanking, SIMAccount, mawakala wetu wa CRDB Wakala.  Pia mapato yetu yameongezeka kufutia kuongezeka kwa pato litokanalo na ubadlishaji wa fedha za kigeni”  amesema Nsekela. 

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio hayo, Nsekela alisema: “Tunajivunia ukweli kwamba tupo kwenye uelekeo mzuri kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea. Lengo si kuyafikia tu, bali Tunakusudia kuyavuka. Tutaongeza kasi zaidi ya utendaji hususani  katika ubunifu na utoaji wa huduma za kidijiti zenye ubora wa juu. Tutaendelea  kuimarisha na kupitia mara kwa mara mifumo yetu ya utoaji huduma  kwa wateja ili kuhakikisha kuwa tunakidhi mahitaji ya soko.”
Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni na Mahusiano Benki ya CRDB, Tully Esther Mwampamba, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya na Mkurugenzi Rasilimali Watu Benki ya CRDB, Siophoro Kishimbo wakifatikia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Katika kipindi cha Januari mpaka Juni 2019, mapato halisi ya riba ya Benki ya CRDB yaliongezeka kwa asilimia 30% na kufika TZS 258 bilioni kutoka TZS 198 bilioni ziilizokusanywa katika kipindi kama hiki mwaka 2018. Huku rasilimali zikiongezeka kwa asilimia 8% kufikia shilingi 6.38 trilioni kulinganisha ni shilingi 5.93 zilizopatikana katika robo ya kwanza ya mwaka 2019. Pia amana za wateja wetu ziliongezeka kwa asilimia 15% kufikia TZS 4.95 trilioni kutoka TZS 4.32 trilioni zilizopatikana kwa robo ya kwanza ya mwaka huu” alisema Nsekela.

Bwana Nsekela alifafanua kwamba Benki ya CRDB bado inaendelea kuwa na umiliki wa asilimia 22% ya thamani ya soko la mabenki hapa nchini hii kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wenye matawi 238, mashine za kutolea fedha 553 na Mawakala Zaidi ya 10,064 wa CRDB Wakala.

Maeneo muhimu ya ufanisi hadi kufikia Juni  2019
Amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 15%  na kufika TZS 4.95 trilioni kutoka TZS 4.32 trilioni kwa robo ya kwanza ya mwaka
Rasilimali za benki ilikua kwa asilimia 8% na kufika TZS 6.38 trilioni kutoka TZS 5.93 trilioni kwa robo ya kwanza ya mwaka.
Mapato ya riba yaliongezeka kwa asilimia 14% na TZS 315.4 bilioni kutoka TZS 276.8 bilioni za kipindi kama hiki mwaka 2018.
Mapato halisi ya riba yaliongezeka kwa asilimia 30% na kufika TZS 258 bilioni kutoka TZS 198 bilioni za kipindi kama hiki mwaka 2018.
Faida ghafi iliongezeka kwa asilimia 98% na kufikia TZS 86.6 bilioni kutoka  TZS 43.8 bilioni kipindi kama hiki mwaka 2018.
Faida halisi (baada ya kodi) ilikua kwa asilimia 108% na  kufikia TZS61.1 bilioni ikilinganishwa na TZS 29.3 bilioni kipindi kama hiki mwaka 2018.
No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad