MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , leo (jana)
amekabidhi vifaa vya kujifungulia wakina mama (Delivery Pack) katika
Hospital za jijini hapa ikiwa ni sehemu ya kuwasaidia wa kimama wenye
hali hiyo.
Hospital zilizopatiwa vifaa hivyo ni Mnazi mmoja iliyopo Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala,ambapo imepewa vifaa hivyo 300 na zile zilizopo
katika Halmashauri ya Kigamboni.
Akizungumza na wauguzi katika hospitali hiyo,Mstahiki Meya Mwita
aliagiza kuwa vifaa hivyo vitolewa bure kwa wakina mama wenye uhitaji
na kuagiza hospital hizo zisiwauzie.
Alifafanua kuwa wakina mama wajawazito wanapaswa kuthaminiwa na kwamba sio wote wenye uwezo wa kununua vifaa hivyo na kushauri wenye uwezo kuwasaidia.
Alifafanua kuwa serikali kwa kiasi kikubwa imekuwa ikijali wakina mama wajawazito na kushauri kuwa kama wadau wa maendeleo wanapaswa kushirikiana na serikali kuwalinda wa mama wajawazito.
“ Ukiangalia serikali inatilia mkazo jambo hili, inajali wakina mama na kuhakikisha kuwa wanajifungua salama, wote tunapaswa kujali maisha yao, nijukumu letu kulinda mama mjamzito “ alisisitiza.
Changamoto ni nyingi,uhitaji wa vifaa ni mkubwa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wakina mama wanaojifungua,nitoe rai kuwa hili ni jukumu la kila mmoja wetu kuisaidia serikali” aliongeza.
Alisema “Wakina mama ni watu wamuhimu sana katika Taifa hili, tunapaswa kuwaheshimu na kuwathamini, pia wanakazi kubwa ambayo kwao inachangamoto, lakini kama viongozi na wadau wengine tunajukumu la kuwasaidia” alisema Meya Mwita.
“ Vifaa hivi najua havitoshi kulingana na Idadikubwa mliyonayo katika
Hospitali hii, ila niwaombe muwapatie bure msiwauzie, huu ni msaada
kwao, napindi tutakapopata nyingine tutawaletea” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Meya Mwita ameipongeza hospitali hiyo kutokana
na huduma wanazozitoa na hivyo kuwasihi kuendelea na utoaji mzuri wa
huduma hiyo.
Mganga Mfadhiwi wa Hospitali hiyo Sophinias Ngonyani alimpongeza
Meya Mwita kwakutoa vifaa hivyo na kusema kuwa zitawasaidia wakina
mama na kusisitiza kwamba watazigawa bure kama walivyoagizwa.
Alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikihudumia wakina mama wajazito
kutoka sehemu mbalimbali jijini hapa kwani hali hiyo imetokana na
huduma nzuri wanazozitoa.
Aliongeza kuwa hospital hiyo inazingatia utoaji huduma bora kama
ambavyo serikali inasisitiza kila wakatii jambo ambalo alisema
limepelekea kuwa na idadi kubwa ya wakina mama wanaojingulia katika
hospitali hiyo.
“ Tunampongeza Mstahiki Meya kwa kutupatia vifaa hivi, tunauhitaji
mkubwa kulingana na idadi ya wakinamama wanaojifungua hapa kwetu,
ametusaidia sana tunampongeza” alisema.
Hata hivyo vifaa hivyo vitaendelea kutolewa kwa hospitali nyingine
zilizopo jijini hapa ,huku nyingine zikichukuliwa katika ofisi ya
Mstahiki Meya.
Vifaa hivyo vimetolewa na Mstahiki Meya wa jiji kwa kushirikiana na
Kampuni ya usafirishaji abiria kwa njia ya mtandao ya Bolt vyenye
thamani ya shilingi milioni 25.
No comments:
Post a Comment