ALIYELAZWA MWAKA MMOJA MLOGANZILA APATIWA MASHINE YA KUPUMUA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 10 July 2019

ALIYELAZWA MWAKA MMOJA MLOGANZILA APATIWA MASHINE YA KUPUMUA

Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, imempatia msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) Bw. Hamad Awadhi kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yanamlazimu kutumia mashine ya oxygen muda wote ili aweze kupumua.

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH-Prof. Charles Majinge amesema hospitali imempatia msaada Bw. Awadhi kwa lengo la kuokoa maisha yake sanjari na kuimarisha afya yake lakini pia kumuwezesha kuendelea na shughuli zake za kawaida ili kutokua tegemezi kutokana na hali yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru ameeleza kwamba mashine hiyo inathamani ya shilingi milioni tatu na nusu imenunuliwa na Hospitali ya Mloganzila ambapo wataalam wamempatia mafunzo Bw. Awadhi namna ya kuitumia na kuitunza ipasavyo.

Prof. Museru amemtaka Bwan. Awadhi kuitunza na kuitumia vema mashine hiyo kama ambavyo ameelekezwa na wataalam ili afya yake itakapoimarika iweze kusaidia watanzania wengine.

"Hospitali imekupatia msaada wa mashine hii ya kukusaidia kupumua- kwa lengo la kuhakikisha afya yako inaimarika zaidi hivyo tunaomba uitunze na utakapopona kabisa utairejesha hospitali ilituwasaidie wengine" amesema Prof. Museru.

Naye Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri amesema, Bw. Awadhi kwa muda wote aliokuwepo hospitalini ameishi kwa kutegemea mashine ya oxygen ambayo inamsaidia kupumua ambapo kwa siku alikua akitumia gesi wastani wa lita 5,760.

Bw. Hamad Awadhi alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila Julai 9 mwaka 2018 na kuruhusiwa Julai 9 mwaka 2019 baada ya afya yake kuimarika.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Charles Majinge (kushoto) akimpatia msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) Bw. Hamad Awadhi ambaye alilazwa kwa muda wa mwaka mmoja katika Hospitali ya Mloganzila.
 Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi MNH- Mloganzila Redemptha Matindi (aliyevaa gauni la bluu) akitoa maelezo namna mashine ya oxygen inavyounganishwa ili iweze kutumika kwa mgonjwa, anayemfuatia ni Prof. Charles Majinge, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Mohamed Mohamed, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru.
 Prof. Lawrence Museru (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MNH Prof. Majinge (wa pili kuli) kuhusu ununuzi wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) ambayo imegharimu shilingi milioni tatu na nusu, kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
  Dkt.  Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri (kulia) akizungumzia kuhusu matibabu aliyopatiwa Bw. Awadhi kwa kipindi chote alichokua amelazwa hospitalini. 
 Hamadi Awadhi akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Muhimbili-Mloganzila kwa huduma aliyoipata na kwa kumpatia msaada ambao utamuwezesha kuendelea na shughuli zake za kawaida.
 Mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) ambayo amepatiwa msaada Bw. Hamad Awadhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad