HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 10, 2019

Balozi Seif afanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akisalimiana na Mgeni wake Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung aliyefika Ofisini kwake kwa mazungumzo.
 Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung Kulia akiongozwa na Mwenyeji wake Balozi Seif kuelekea Ukumbi wa Mikutano kwa mazungumzo yao Rasmi.
  Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung akitia saini Kitabu cha wageni mara tu baada ya kufika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Ujumbe wa Vietnam ukiongozwa na Waziri Mkuu wake Bwana Trinh Dinh Dung ukifanya mazungumzo na Ujumbe wa Zanzibar ulioongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
 Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung Kushoto akisisitiza ahaja ya nchi yake na Tanzania kuendeleza Uhusiano wa Kibalozi katika Nyanja za Kiuchumi zaidi badala ya Siasa.

 Bwana Trinh Dinh Dung Kushoto akimpatia zawadi Balozi Seif mara baada ya Mazungumzo yao ya Kidiplomasia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga.

 Balozi Seif akimpatia Bwana Trinh Dinh Dung zawadi ya kasha ikiwa ni kumbu kumbu ya ziara aliyoifanya na Ujumbe wake Visiwani Zanzibar.
   Balozi Seif wa Tano kutoka Kulia pamoja na Mgenzi wake Bwana Trinh Dinh Dung akiwa Kulia yake wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Ujumbe wa Zanzibar na Vietnam.
Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha na – OMPR – ZNZ.

Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung alisema uhusiano wa Kidiplomasia uliyopo baina ya Mataifa ya Vietnam na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa unastahiki uelekezwe katika masuala ya Uchumi na Biashara.

Alisema uhusiano huo ulikuwa amejikita zaidi katika masuala ya Kisiasa hasa ikizingatiwa kwamba wakati huo ulikuwa kipindi cha mpito cha Mataifa hayo kutokan katika mikono ya Tawala za kikoloni.

Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar akiwa Nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya Siku Nne.

Alisema Sekta za Uchumi na Biashara kwa sasa kutokana na mabadiliko ya Dunia ndio fursa pekee itakayoendelea kuunganisha pande hizo mbili kupitia maingiliano ya Taasisi za Umma na hata sekta binafsi ya Watu wa Mataifa hayo mawili rafiki.

Bwana Trinh Dinh Dung alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kwa sasa ipo haja ya kuundwa kwa Kamisheni ya pamoja kati ya Tanzania na Vietnam itakayotoa muelekeo wa kufanikisha ustawi wa Wananchi wa pande hizo mbili.

Alisema umadhubuti wa Kamisheni hiyo itakayopaswa kuhusisha Wataalamu, Wafanyabiashara na Watu maarufu unaweza kuibua Miradi ya Kiuchumi na kutoa fursa ya Uwekezaji kwa Makampuni na Wafanyabiashara wa Vietnam na Tanzania.

Bwana Trinh Dinh Dung alishauri kwamba masuala hayo ni vyema yakaenda sambamba na Mabadiliko ya Viwanda yaliyopo Ulimwenguni hivi sasa ambayo yatachangia kutoa ajira nyingi hasa kwa makundi ya Vijana na Wanawake.

Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Nchi yake iko tayari kubadilishana uzoefu a Utaalamu katika hatua ya kuelekea kwenye Maendeleo.

Alifahamisha kwamba yapo maeneo ya kushirikiana katika kuimarisha Uchumi akiyataja baadhi kuwa ni pamoja na Sekta ya Utalii ambayo Zanzibar tayari imeshajiimarisha kuwa kituo maarufu cha kuunganisha safari za Watalii Ulimwenguni.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar na Vietnam zinafanana katika harakati zao zilivyokuwa wakati wa kudai Uhuru.

Balozi Seif alisema ziara za Viongozi Wakuu, wale Waandamizi pamoja na Wataalamu wakiwemo pia Wafanyabaishara za kutembeleana zinaweza kuongeza ukaribu zaidi wa ushirikiano wa pande hizo mbili rafiki.

Alisema Zanzibar na Tanzania kwa jumla imeweka Milango wazi kwa Wawekezaji wa Nje kuanzisha Miradi ya Kiuchumi ambapo aliwaomba Wawekezaji wa Vietnam kupitia Kiongozi wao huyo kuitumia fursa hiyo.

Balozi Seif alieleza kwamba inapendeza kuona kwamba Timu ya Wataalamu kutoka Vietnam imeshafika Zanzibar Miaka ya nyuma kusaidiana na Wataalamu Wazalendo kufanya Utafiti katika Sekta za Baharini na Kilimo, Utafiti ambao unaweza kuleta tija hapo baadae.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Vietnam kwa jitihada inazochukuwa za kuendelea kuiunga Mkono Zanzibar Kitaalamu katika Sekta tofauti za Maendeleo.

Vietnam na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimeanza ushirikian o wa Kidiplomasia mnamo Mwaka 1965 ambapoMataifa yote mawili yameshasini Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya Uchumi, Biashara, Sayansi na Teknolojia.

Ziara ya Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam Bwana Trinh Dinh Dung itakayomchukuwa siku Nne imeanzia Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE}, Tanzania na pia itamalizia Umoja huo wa Fame za Kiarabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad