HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 21, 2019

HDIF, UKaid na COSTECH kukutanisha wadau wa ubunifu kujadili, kukuza na kuendeleza ubunifu

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MFUKO wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Binadamu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeandaa wiki ya ubunifu inayotarajia kuwaleta pamoja wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa ili kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini.

Wiki hiyo ya ubunifu,  imelenga kuwakutanisha wataalamu, watafiti na wabunifu  ili kujadiliana namna ya kukuza na kuendeleza masuala ya ubunifu nchini.

Wiki hiyo, itakayoanza Machi 25-30 mwaka huu,  inafanyika kwa mara ya tano nchini Tanzania  ambapo mwa huu,  imefanikisha kuwafikia mpaka wadau walio nje ya Dar katika Mikoa ya Iringa na Arusha tofauti na awali ambapo wiki hii ilikuwa ikifanyika Dar es Salaam pekee.

Akizungumza na wanahabari leo Machi 21.2019 Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu amsema kauli mbiu ya wiki ya ubunifu mwaka huu ni ya kukuza na kuendeleza Bunifu kwa maendeleo ya Watu'. Ambapo amesema  Tume  kupitia Mfuko wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia wamefungua milango kwa wabunifu mbalimbali na kutoa fursa za kuendeleza ubunifu nchini.

Amesema, kwa kushirikiana na HDIF na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA), wametoa Sh bilioni 1.9 kwa wabunifu bora 32 na kumbi za Bunifu 15, zilizoshinda mashindano ya COSTECH ya mwaka 2018.

Dk. Nungu ameongeza kuwa,  wameandaa utaratibu wa kuwatambua wabunifu wote nchini na kuweka kwenye makundi kulingana na viwango vya ubunifu wao "Mwanzoni mwa mwezi Machi, tume ilifanikiwa kuratibu mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) ambapo wabunifu 60 walichaguliwa kiushandani katika nyanja mbali mbali.

Ameongeza, kwa miaka mitano mfululizo HDIF na COSTECH wamekuwa wakishirikiana kuinua ubunifu nchini kupitia sekta za afya, maji na elimu na kuboresha mfumo mzima wa ubunifu ikiwemo uwezeshaji na miundombinu.

"Tunalenga Tanzania kuwa na mfumo thabiti wa ubunifu kwa kuhakikisha kuwa wabunifu, wataalamu mbalimbali na jamii inakutana ili kujifunza vitu ambavyo wabunifu hao wanavifanya," amesisitiza.

"Maonesho haya yanatoa fursa kwa wabunifu, watafiti kutoka vyuo vikuu nchini, wajasiriamali na jamii kwa ujumla kuona namna ya kukuza uchumi wa viwanda kupitia ubunifu kwani katika kutekeleza lengo la kufikia uchumi wa viwanda, sekta yetu ya ubunifu yenyewe ina mchango mkubwa kwani inazalisha ajira na kutangaza bidhaa zetu ndani na nje ya nchi," amesema

Alisema maboresho ya mwaka huu ya ubunifu yatawaunganisha wadau wa sekta binafsi, wafanyabiashsra, serikali na wabunifu ili kushirikiana kuingiza bidhaa za ubunifu sokoni lengo ni kukuza uchumi wa viwanda kwa uhalisia.

Kwa upande wake, Kiongozi Mkuu wa HDIF, David McGinty amesema katika kipindi cha miaka mitano ya uendeshaji wa ubunifu huo, matokeo chanya yamejidhihirisha kwa   ongezeka la washiriki kukuza kwa zaidi ya asilimia 50 na Tanzania inaonekana ikipanda kwa nafasi 31 huu katika rekodi za kipimo cha Ubunifu cha Dunia.

Aidha amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo ili kuona kazi zinazofanywa na watanzania katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kupitia ubunifu.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller amesema wiki hiyo inatoa fursa kwa wabunifu, wafadhili na sekta binafsi kubadilishana mawazo na kuhamasisha masuala ya ubunifu.

Amesema, wadau watakaoshiriki katika maonesho hayo ni Digital Impact Alliance (DIAL), Ubalozi wa Uswisi, 10 School of TECH, Buni, Ndoto na Digital Opportunities Trust na wengine watakaoendesha maonesho hayo.

Ameongeza, katika wiki hii ya ubunifu kutakuwa na shughuli zaidi ya 60 ambazo zitakuwa zikiendelea kwa pamoja na maonyesho 30 katika kumbi kuu za COSTECH na Dlab Kijitonyama Sayansi. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu wa katikati akizungumza na waandishi wa Habari  juu ya wiki ya ubunifu itakayoganza Machi 25-30 mwaka huu ambapo wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa na wanatarajiwa kukutana pamoja kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini. Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller na kushoto ni Kiongozi Mkuu wa mfuko wa ubunifu wa maendeleo, (HDIF)David McGinty.
 Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano huo ambapo amesema wiki hiyo inatoa fursa kwa wabunifu, wafadhili na sekta binafsi kubadilishana mawazo na kuhamasisha masuala ya ubunifu.
 Kiongozi Mkuu wa mfuko wa ubunifu wa maendeleo, (HDIF)David McGinty  ambao ndio waandaaji wa wiki ya ubunifu akifafanua jambo kwa waandishi wa  Habari juu ya wiki hiyo ambayo25-30 ambayo inatarajia kuwaleta pamoja wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa ili kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu alipokuwa akieleza dhima ya ya wiki ya ubunifu itakayoanza Machi 25-30.2019  ambayo inatarajia kuwaleta pamoja wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa ili kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad