HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 21 March 2019

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA LA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE), Machi 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE), Machi 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Tanzania Mstaafu, Bibi Helen Kijo Bisimba baada ya kufungua Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE) Machi 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

WAZIRI mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wadau kuunganisha juhudi za pamoja kukabiliana na ukatili dhidi ya makundi ya wanawake na watoto.

Hayo yamesemwa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Majaliwa amesema serikali imeandaa mwongozo na utaratibu wa usimamizi na ufuatiliaji unaotoa maelezo kuhusu uundwaji wa kamati mbalimbali za mfumo wa mawasiliano na uwasilishaji wa taarifa.

“Lengo kuu la serikali ni kuhakikisha ukatili dhidi ya wanawake na watoto na makundi kengine unatokomezwa na haki zote zinalindwabna kuheshimiwa,”amesema Majaliwa.

Pia, amesema kutakuwa na kamati za kijinsia na ustawi wa wanawake na kwenye kuunga mkono serikali imefanya jitihada mbalimbali za kufanya kampeni za kitaifa ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni ikiongozwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa mtoto (CDF).

“Suala la ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni jambo mtambuka na linahitaji ushitikishwaji wa wadau katika kutokomeza janga hili linaloikabili nchini yetu.”amesema Majaliwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF)Bwn Koshuma Mtengeti ameiomba serikali kutoa ushirikiano pamoja na kutenga bajeti ya kutosha katika kuendesha mikakati ya kupinga ukatili wa kinjisia nchini.

"Mwezi Mei mwaka 2018, mwalimu wa shule ya msingi hapa jijini Dar es Salaam alituhumiwa kuwadhalilisha kingono wanafunzi wake wanne wa kike wa darasa la saba kwa kuwageuza kuwa wake zake na kufanya nao ngono,”amesema Mtengeti.

Tunakushukuru sana Mh. Raisi John P. Magufuli kwa salamu zako kutoka kwa Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa. Tumefarijika kujua kwamba uko nasi bega kwa bega katika kongamano hili la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Prof. William Anangisye amesema Suala la Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake ni nyanja pana, ni tatizo linalozikabili nchi zote Duniani ingawa viwango vya Ukataili hutofautiana.

Ripoti mbalimbali za haki za binadamu zimeweza kuonyesha kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha mwaka 2018 ukilinganishwa na mwaka 2017 nchini.

Aidha, kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kudadavua ukubwa wa sura za ukatili yanayowasibu wanawake na watoto  na litasaidia juhudi za kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia, kukabili na kuanzisha utaratibu wa kuboresha huduma kwa watoto na wanawake waathirika wa ukatili.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad