HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 9 February 2019

Wananchi watakiwa kushiriki katika kufanikisha elimu kwa wasichana

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dr. AveMaria Semakafa ameitaka jamii kuzingatia utoaji na upatikanaji wa elimu kwa kuhakikisha kwamba wanaboresha mazingira yake.
Akizungumza katika kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, alisema maelekezo mpya kuhusu elimu yanahitaji ushirikishaji wazazi katika kila jambo kwa lengo la kuwezesha utekelezaji wa sera ya elimu.
Mpango huo unaotekelezwa kwa majaribio katika wilaya za Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Mkoani kisiwa cha Pemba.
Alisema kwa sasa kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo wakaguzi wamepewa namna mpya ya ukaguzi wa maendeleo ya shule ikiwa ni pamoja na kuangalia majirani na wazazi.
Alisema ingawa kwa sasa wavulana ndio wanaocha shule kwa wingi kuliko wasichana, serikali imekazania wasichana kwa sababu mara zote msichana anapokwama kuendelea na shule huwa ndio mwisho wa ndoto zake.
“Watoto wa kiume wanaacha sana shule kuliko wasichana, lakini hawa huacha na kujitumbukiza katika fursa mbalimbali za kiuchumi, lakini wasichana wakikwama inakuwa ndio mwisho wao” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Hata hivyo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano kazi huo alisema kwamba tatizo la utamaduni linafanya maamuzi mengi katika namna ya kuokoa mtoto wa kike hapa nchini kuwa na sababu za kutofautiana.
Alisema wasichana wengine wanaacha shule si kwa sababu ya mimba, lakini ni kutokana na umbali wa shule na mazingira magumu ya kupata elimu hiyo; pia kuwapo kwa mabadiliko ya kimwili kwa kuzingatia asili ambayo humkatisha mwanamke siku 4 au sita kuhudhuria masomo kila mwezi.
Aidha alisema tatizo jingine ni saikolojia iliyoambatana na utamaduni ambapo wasichana wengi hushawishiwa na wazazi wao kutofanya vyema ili wasiendelee na shule.
Alisema kutokana na ukweli huo serikali imeanzisha kampeni ya kujenga hosteli na madomitori kwa ajili ya wasichana ili kuwapunguzia adha ya usafiri kwa kuangalia mazingira yao.
Alisema ingawa serikali inafahamu shida iliyopo kwa watoto wa kiume, kwa sasa mkazo uko kwa mabinti na baadae ndio wanaume.
Alisema hata hivyo kwamba serikali ya Tanzania inajikita zaidi katika kuhakikisha kwamba inatoa elimu ya msingi yenye ubora kwa wananchi kwa mujibu wa sera ya mwaka 2014 na kuwashukuru wadau kwa kuchangia katika kuimarisha elimu hiyo.
Alisema mipango mingi ya wadau ikiwemo ya kusoma kwa njia ya mtandao, mpango ulioanzishwa Ngorongoro sasa unafaa kusambazwa maeneo mengine yenye ugumu kama wilaya ya Igunga ambapo baadhi ya wanafunzi hulazimika kutembea kilomita 15 kufuata shule.
Pia alisema mradi kama huo wa kuwezesha mabinti unatia shime katika juhudi za serikali kuwakomboa wanawake na kwamba kazi inayofanywa na wadau ni ya kufanikisha sana.
Mradi huo unashirikisha mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNESCO, UNFPA, UN Women umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA).
Katika mkutano huo kulijadiliwa ripoti za utekelezaji wa mradi kwa mwaka jana, matokeo yake na kupanga kazi za mwaka huu.
 Mwenyekiti wa semina ya kuwawezasha wasichana na wanawake katika elimu Tanzani, Dr. Ave Maria Semakafu (kushoto) ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akifungua kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos.
 Naibu Mkurugenzi wa KOICA Tanzania, Inae Kim akifuatilia taarifa ya kamati ya kuwawezesha wasichana na wanawake katika elimu Tanzania wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dkt. Edicome Shirima (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos (wa pili kushoto) akichangia mada wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina ya kuwawezasha wasichana na wanawake katika elimu Tanzani, Dr. Ave Maria Semakafu ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
 Msimamizi wa mradi wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA, Bi. Viola Kuhaisa akiwasilisha taarifa kwa washiriki wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu kilichofanyika katika Hotel ya Courtyard jijini Dar es Salaam
Washiriki wakisikiliza taarifa iliyowasilishwa na UNESCO wakati wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja ya wadau na waandaaji wa kikao cha pili cha kamati ya kitaifa ya mpango wa pamoja wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupitia elimu, unaofanywa kati ya serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ufadhili wa KOICA kilichofanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa semina ya kuwawezasha wasichana na wanawake katika elimu Tanzani, Dr Ave Maria Semakafu ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi katika picha na bango la mradi huo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad