HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 9, 2019

MASAUNI AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA TAASISI ZA KIISLAM JIJINI DAR ES SALAAM

Serikali imesema haitakua tayari kuona Amani na Utulivu wa Nchi inachezewa huku ikisisitiza uwepo wa Umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifungua Semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwahusisha Viongozi wa Taasisi za Kiislamu lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao

Amesema muelekeo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini lengo ikiwa kuinua maisha ya wananchi nan chi kwa ujumla

“Serikali hii imejidhatiti kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi na maendeleo hayawezi kuja ikiwa amani na utulivu haupo, sisi kama serikali tutahakikisha tunalinda amani iliyopo ili wananchi wapate kufanya shughuli za kiuchumi bila wasiwasi wowote” alisema Masauni

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum aliihakikishia serikali kutokuwepo kwa mifarakano kati ya taasisi mbalimbali kama ilivyokuwepo awali huku akisisitiza kuendelea kwa umoja huo ili jamii ipate kuendelea

“Sisi kama Bakwata tunaihakikishia serikali uwepo wa umoja na ushirikiano baina ya baraza na taasisi zingine na tofauti zetu hazipelekei kukoseana au kuvunjiana heshima kwahiyo tunaomba serikali iamini uwepo wa maelewano mazuri tu kwa maendeleo ya nchi hii” alisema Sheikh Mussa

Semina hiyo ya Siku mbili imejumuisha viongozi wa Taasisi mia moja huku mada ya Nafasi ya Taasisi za Kiislam katika Kuleta Umoja na Kuishi kwa Amani itajadiliwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo aliwahakikishia uwepo wa Amani na Utulivu nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo aliihahakikishia serikali kuwepo kwa maelwano kati ya taasisi mbalimbali za dini lengo ikiwa ni kurahisisha maendeleo nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akisalimiana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo aliwahakikishia uwepo wa Amani na Utulivu nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad