HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 1, 2019

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA, APOKEA MADARASA MAWILI YA SHULE YA SEKONDARI KASSIM MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa jana Desemba 31, 2018 alizindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa pamoja na kupokea madarasa mawili yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa kwa udhamini wa Benki ya CRDB, iliyopo katika Kijiji cha Kilimahewa.
Waziri Mkuu aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kufanikisha kujenga tawi hilo ambalo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi wa Ruangwa kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki.
Kadhalika, Waziri Mkuu alisema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018. Wengine pichani ni kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa, Method Muganyizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay wakifungua pazia katika kibao kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018. Wengine pichani ni kutoka kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Ruangwa, Method Muganyizi. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Desemba 31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa yaliyojengwa na Benki ya CRDB, iliyopo katika Kijiji cha Kilimahewa, Ruangwa mkoani Lindi Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakiwa wameketi katika madeski pamoja na baadhi ya wanafunzi katika moja ya madarasa hayo yaliyojengwa na Benki ya CRDB.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad