HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 9 January 2019

VIGOGO KAMPUNI YA VKP INVESTMENT FOUR YOUTH WAFIKISHWA KORTINI KWA KUJIPATIA MILIONI 300/- KWA NJIA YA UDANGANYIFU

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 
Mkurugenzi wa kampuni  ya VKP Investment Four Youth, David Manot, mwanasheria wa kampuni hiyo Ernest Ngonyani na wenzao wanne wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa mashtaka 31 ya' kujipatia zaidi ya sh.milioni 300 kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la kula njama.

Washtakiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo pamoja na Manot ni, mfanyabiashara, Yona Kiita, Mkurugenzi wa masoko, Jane Isack, Afisa Masoko, Modikai Kilala na Meneja muendeshaji Juliana Kasambala. Mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando, imedaiwa na wakili wa serikali Ester Martin kuwa kati ya Januari 2016 na Desemba 2018 katika jengo la Mwalimu House lililopo Katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. 

Katika mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu washtakiwa wote hao wanadaiwa kati ya Novemba 21, 2017 na Aprili mahali hapo hapo, washtakiwa kwa nia ya kutenda kosa walijipatia fedha kupitia kampuni hiyo ya VKP investment for Youth kutoka kwa Anna Kavishe kwa kujifanya kuwa wangemuuzia kiwanja huku wakijua kuwa siyo kweli.

Washtakiwa hao wanadaiwa kupata kiasi tofauti tofauti cha pesa kutoka kwa Joel Olinda, Mlolu Chelehan, Shukuru Olomi, Emmanuel Mlambity, Agnes Joseph,  Christopher Mraha, Prowin Mtei, Mustapha Ngayoma,Chausiku Kinyehe, Issa Illy, Samson Ngayoma, Asha Mtangaza, Prisca Mrope Dotto Pangimoto, Nice Mohammed, Elizabeth Makombe na Elirehema Mangore.

Wengine ni, Mgaza William, Nataka Milivya, Joyce Chacha, Diana Mussa, Lucy Mpayo, Benson Mboya, Comfort Peter, Ilenedy Bongezi, Edwin Mwimbula, Emmanuel Messy, Azizi Mohammed na Anna Tarimo.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande hadi January 11, 2019 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutolewa maamuzi  juu  ya dhamana ya washtakiwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad