HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 9 January 2019

RAIS DKT.SHEIN AFUNGUA SKULI YA SEKONDARI NA MSINGI BWEFUM WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kuifungua Skuli ya Seokndari na Msingi ya Bwefum Wilaya ya Magharibi B Unguja kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto Waziri wa Elimu na Mafunzio ya Amali Zanzibar Mhe. Rizi Pembe Juma,Skuli hiyo imejengwa na Kampuni ya Union Property Developers Ltd, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Kisasa ya Sekondari na Msingi ya Bwefum, Wilaya ya Magharibi B Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuwahutubia Wananchi na kuifungua rasmin Skuli hiyo.
(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkandarasi aliyejenga Majengo ya Skuli hiyo kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Quality Bulding Contractors Ltd. Mkurugenzi ,Mtendaji  Ndg. Shaib Said Ali, akitowa maelezo ya Majenzo ya Skuli hiyo yaliotengenezwa na Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Bwefum Kidatu cha Tatu Khamis Masoud.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, wakati Rais wa Zanzibar akitembelea moja ya Madarasa hayo alipotembelea baada ya kuifungua rasmin Skuli hiyo, ikiwa ni shamrashamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Bwefum Wilaya ya Magharibi B Unguja Masoud Mussa, Naifat Makame na Suleiman Sapu, wakiimba wimbo wa "Sisi Sote Tumegomboka " wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Skuli yao, iliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,. Dk. Ali Mohamed Shein, Skuli hiyo imejengwa na Kampuni ya Union   Property Developers Ltd.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad