HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 9 January 2019

TFF KUTANGAZA DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO KESHO0

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii. 

KATIKA mchakato  wa kuendelea kwa michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC)  Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  imetangaza kuwa itafanya droo ya Kombe hilo siku ya kesho Januari 10 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Hababari katika ofisi za TFF jijini Dr es Salaam. Afisa habari wa TFF Cliford Ndimbo amesema, droo hiyo itakafanyika katika Makao Makuu ya Azam Tv, iliyopo Tabata majira ya saa 5 asubuhi na itahusisha raundi ya 4 zenye timu 32 na raundi ya 5 itakayohusisha timu 16.

Ndimbo amesema timu zilizobaki katika hatua hiyo ni  Young Africans SC, Azam FC, Lipuli FC, Mtibwa Sugar, KMC, Coastal Union, Kagera Sugar, Mbeya City, Stand United, JKT Tanzania.

Nyingine ni Singida United, Alliance FC, African Lyon, Biashara United, Boma, Namungo, Mbeya Kwanza, Friends Rangers, Majimaji FC, Dodoma FC, Pamba SC, Rhino Rangers, Reha FC, Dar City, Polisi Tanzania, Mashujaa, Transit Camp, The Mighty Elephant, Cosmopolitan, Kitayosce, La Familia FC, Pan African

Ameongeza, mshindi atakaeibuka katika mashindano  hayo ataipeperusha bendera na  kuwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, ambapo mwaka jana Mtibwa Sugar ndio waliibuka kidedea wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad