HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 December 2018

WAMACHINGA KUBADILI SURA YA MKOA WA SINGIDA

Na Sixmund J. Begashe
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi, amesema Mkoa wa Singida unatarajia kuwa wa mfano nchini kwa upande wa maendeleo yatakayo letwa na wafanya biasha wadogo wadogo wajulikanao kama wa Machinga.
Mh Nchimbi ameyasema hayo kwenye shughuli ya kuwatunuku vyeti vya mafunzo ya MKURABITA pamoja na kukabidhi vitambulisho  vilivyo tolewa na Mh Rais Dr Magufuli kwa wafanya biasha wadogo zaidi ya mia sita walio udhuria mafunzo maalumu ya ujasiria mali yaliyoendeshwa na Taasisi ya MKURABITA Mkoani Singida.
Katika zoezi hilo Dr Nchimbi aliwaeleza wajasiria mali hao kuwa Vitambulisho hivyo ni ishara tosha kuwa Mh Rais Magufuli anaupendo mkubwa dhidi ya watanzania wote hasa wananchi wenye vipato vya chini na walie wanyonge hivyo ipo haja kubwa kwa wamachinga nao  kuonesha kupokea heshma hiyo kwa kufanya kazi kwa bidi ili waje kuwa wafanya biasha wakubwa na walipa kodi wazuri. 
" Heshma aliyotupa Mh Rais Dr John Pombe Magufuli sisi Mkoa wa Singida kupitia ninyi wafanya biasha wadogo wadogo ni kubwa sana, hivyo tunapashwa kuitendea haki heshma hii kwa kuhakikisha tunafanya biashara zetu kwa weledi mkubwa na juhudi ili tupande na kuwa wafanya biashara watakao lipa kodi kwa maendeleo zaidi ya Mkoa wetu na nchi kwa ujumla."Dr Nchimbi alisema
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa aliwaonya watumishi wa umma wenye tabia ya kuwabughudhi wafanya biashara ndogondogo Mkoani humu kuacha maramoja hasa pale watakapo waona wafanya bihashara hao wamevaa vitambulisho vyao halali vilivyo tolewa na Mh Rais Magufuli.
Licha ya kuzungumzia utaratibu wa namna ya kuvipata vitambulisho hivyo vinavyo simamiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa TRA Mkoa wa Singida Bw Apili Mbaruku alionya wafanya biasha wakubwa wenye tabia ya  kuwatumia wa machinga  watakao pewa vitambulisho hivyo ili kuwauzia bidhaa zao kwani kwa kufanya hivyo nikosa kisheria na hivyo sheria itachukuwa mkondo wake.
Mkurugenzi wa Raslimali na Biashara wa MKURABITA Bw Japhet Werema licha ya kuelezea mafanikio ya mafunzo hayo pia ameelezea malengo ya mafunzo hayo ni  kuwapatia elimu wafanya biasha wadogowadogo wa Mkoa wa Singida ili wawe na uwelewa mpana wa mambo ya kibiashara  kupitia vyombo mbali mbali vinavyo husika kama Mabenki, BRELA, TRA n.k
Nao wafanya biashara waliopatiwa vitambulisho hivvyo akiwemo Bi Zakia Muna walionesha furahaa yao kwa kumshukuru Mh Rais Mgufuli kwa upendo mkubwa wa kuwajali kwa kuwapatia vitambulisho ambavyo kwao ni kama mkombozi kutoka kwenye kukimbizana na mgambo kila kukicha hivyo kwa sasa watafanya kazi zao wakiwa huru.
"Mkuu wetu wa Mkoa ametuombea na kutupa baraka zote na kutuambia kuwa hata Mbuyu ulianza kama Mchina, hakika na mimi kwa kupitia kitambulisho hiki, na kwa kuwa nitafanya biashara zangu kwa amani, siku si nyingi nami nitakuwa mfanya biasha mkubwa na nitaanza kulipa kodi ili nchi yangu ipate maendeleo makubwa, namshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kutupatia vitambulisho hivi kwa haraka sana." Bi Muna alimalia.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akionesha mwonekano wa vitambulisho vilivyo tolewa na Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano  kama Wamachinga Mkoani Singida, pembeni yake ni Meneja wa TRA Mkoa wa Singida Bw Apili Mbaruku.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akiwakabidhi vitambulisho maalumu vilivyo tolewa na Mh Rais Magufuli kwa wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano kama Wamachinga Mkoani Singida.
Baadhi ya wafanya biasha wadogo wadogo wajulikano kama Wamachinga Mkoani Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkua  wa Singida Dr Rehema Nchimbi (ayupo pichani)


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad