HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 December 2018

TAA Kutekeleza Mradi wa Bil. 55 Mkoani Mtwara

Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mtwara utakaogharimu Shilingi Bilioni 55.

Akizungumza moja kwa moja baada ya kuunganishwa mbashara redioni na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela aliwahakikishia wananchi wa Mtwara kuwa kazi ya upanuzi mkubwa wa uwanja huo itaanza.

“Kuna mradi wa takribani shilingi Bilioni 55 kupanua Uwanja wa Ndege wa Mtwara na kazi inakwenda kuanza.Pia kuna kazi za ukarabati Uwanja wa Songea na Nachingwea yote ni katika kulifungua eneo la Kusini," alisema. Aidha, Mayongela Alisema kuwa mradi huo una lengo la kuimarisha kuimarisha usafiri wa anga katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ili kuiunganisha na mikoa mingine.

Mayongela aliongeza kuwa Mradi huo utatekelezwa na mkandarasi kutoka China na tayari yupo katika eneo la mradi Kwa upande wake Dkt. Abbasi amesema kuwa  Serikali itaendelea kuhakikisha inazijenga na kuziboresha barabara za vijijini kupitia Taasisi ya TARURA iliyopewa jukumu la kusimamia eneo hilo.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano Maalum na Radio Safari Fm ya mkoani Mtwara kuhusu miaka mitatu ya utekelezaji katika Serikali ya Awamu ya Tano

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad