Na Leandra
Gabriel, Blogu ya jamii
TAASISI ya
WAJIBU inayojishughulisha na uwajibikaji na utawala bora chini ya
mkurugenzi mtendaji na mkaguzi mkuu mstaafu wa hesabu za serikalini (CAG) Ludovick Utouh imekutana na kufanya majadiliano wa na wadau
wa tasnia ya ya habari na kujadili dhana nzima ya uwajibikaji na utawala bora
na namna ya kuripoti na kuandika makala kuhusiana nayo.
Akisoma
hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji
wa taasisi wa WAJIBU Ludovick Utouh Meneja wa utawala na fedha Jackson Mmary
amesema kuwa mjadala huo ni kati ya taasisi hiyo pamoja ma waandishi wa habari ili kuweza
kujenga taifa na kuongeza uelewa wa wananchi juu ya dhana nzima ya uwajibikaji
na utawala bora nchini.
Ameeleza kuwa
taasisi ya WAJIBU inaamini kuwa uwajibikaji na utawala bora kwa pamoja ni
muhimu sana katika maendeleo ya taifa licha ya kutoelewaka kwa watanzania walio
wengi na kwa namna moja au nyingine wadau mbalimbali wanatakiwa kushirikiana
ili kuweza kuwafikia wananchi na kuhakikisha wanaelewa dhana hiyo ya
uwajibikaji inaeleweka.
Pia amesema
kuwa taasisi hiyo ya WAJIBU inapendekeza taaluma ya habari lazima iwajibike
zaidi kwa umma wa watanzania kwa kuendelea kuripoti kuhusu mambo yote
yaliyoripotiwa huko nyuma yenye umuhimu
mkubwa kwa maendeleo ya wananchi ikiwa ni pamoja na mengi yaliyofanywa na
serikali.
Akieleza majukumu
ya taasisi hiyo amesema Afisa utafiti wa taasisi hiyo Hassan Kisena amesema
kuwa taasisi hiyo ya fikra ya uwajibikaji iliyoanzishwa mwaka 2015 ina majukumu
mengi kubwa ikiwa ni kuangalia uwepo wa
usimamizi mzuri wa rasilimali za umma pamoja na kuandaa ripiti za uwajibikaji
kwa lugha rahisi ya ueleweka kwa wananchi, kuandaa machapisho ya uwajibikaji
kisekta kama vile elimu, afya na maji sambamba na kutoa mafunzo kwa wabunge, madiwani, AZAKI na
mashirika mbalimbali na kuandaa makongamano ya uwajibikaji vyuoni kuhusu
masuala ya kupiga vita rushwa na ufisadi kwa vyuo vikuu nchini ili kuwajenga
wanafunzi hao kukataa na kupinga vitendo vya rushwa.
Amesema kuwa
taasisi hiyo inafanyia kazi mapendekezo mbalimbali yanayotolewa katika ripoti mbalimbali zikiwemo za CAG,
PPRA, TEIT na PCCB kwa kuyaweka kirahisi zaidi na kufanyiwa kazi na amehimiza
kuwa wao kama Wajibu wanaamini kuwa taarifa yenye manufaa makubwa kwa jamii
lazima iripotiwe mfululizo hadi jambo hilo litakapokwisha na baadaye matokeo ya
jambo hilo kutolewa.
Kwa upande
wake Kaimu mkurugenzi mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini kutoka ofisi
ya taifa ya ukaguzi (NAOT) Sarah Reuben amesema kuwa ofisi ya ukaguzi wa hesabu
za serikali (CAG) iliyoanzishwa kikatiba
chini ya ibara ya 143 ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na inazingatia na kusimamia uwajibikaji na
uzingatiaji wa sheria na kuhakikisha watumishi wa umma wanatekeleza majukumu
yao na hayo yoe ni kwa kushirikisha vyombo vya habari.
Bi. Sarah
amesema kuwa ofisi ya Rais inayohusika na utumishi wa umma imetoa miongozo kwa
ofisi za za serikali kuhusisha vtombo vya habari katika utoaji wa ripoti mbalimbali na pia
ofisi hiyo huandaa warsha mbalimbali kwa waandishi mbalimbali na mara zote mnyororo
wa thamani wa ofisi hiyo hukamilika kukiwa na mhimili wa CAG, serikali, bunge,
wadau wa CAG na vyombo vya habari.
Meneja wa Fedha na Utawala kutoka Taasisi ya WAJIBU Jackson Mmary akisoma risala ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU Ludovick Utouh wakati wa ufunguzi wa warsha ya Majadiliano kati ya WAJIBU na waandishi wa habari iliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Utafiti na Miradi kutoka Taasisi ya WAJIBU, Moses Kimaro aikitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika warsha wa Majadiliano kati ya WAJIBU na waandishi wa habari uliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Sarah Reuben akiwasilisha mada kuhusu kazi zinazofanywa na ofisi hiyo kwa waandishi pamoja na wadau wa habari kwenye warsha ya Majadiliano kati ya WAJIBU na waandishi wa habari iliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Afisa Utafiti kutoka taasisi ya WAJIBU, Hassan Kisena akiwasilisha mada kuhusu historia ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo kwa wadau wa habari waliofika kwenye warsha ya Majadiliano kati ya WAJIBU na waandishi wa habari iliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Mwandishi Mwandamizi Vicky Ntetema akitoa uzoefu wake mbele ya wanahabari kuhusiana na dhana nzima ya uwajibikaji na utawala bora katika mkutano uliowakutanisha waandishi wa habari na taasisi ya WAJIBU leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada kwenye warsha ya Majadiliano kati ya WAJIBU na waandishi wa habari uliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment