HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 3, 2018

PROF. MBARAWA AAGIZA UJENZI WA TENKI LA MAJISAFI SARANGA

Waziri wa Maji Mhe. Prof Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kuanza ujenzi wa tenki la Maji safi lenye uwezo wa kuhifadhi Maji kiasi cha lita za ujazo milioni tano katika eneo la Saranga jijini Dar es salaam.

Alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea katika maeneo ya Kimara Temboni na Saranga na kushuhudia changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Maji safi katika maeneo hayo iliyosababishwa na jografia ya milima na kupelekea kuwepo kwa msukumo mdogo wa Maji katika maeneo hayo. Hali hiyo ilikuwa ikisababisha baadhi ya wakazi hao kukosa huduma ya Maji.

“Niwahakikishie kuwa mtapata huduma ya Maji safi kwa masaa 24 na siku saba kwa wiki kama maeneo mengine kwa kuwa nimewaagiza DAWASA wajenge tenki la Maji safi lenye ujazo wa lita milioni tano ambalo lita sambaza Maji katika eneo lote la Saranga. Tayari wameshaanza kazi ya kutafuta mkandarasi na baada ya muda mfupi ujenzi utaanza” alisema Prof. Mbarawa

Aidha kwa upande wa Afisa mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amehaidi kutekeleza agizo la Waziri wa Maji kwa wakati ilikuendana na kasi na adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kumtua mama ndoo ya Maji kichwani kwa kuwafikishia huduma hiyo karibu zaidi  ilikuondokana na kero ya kufuata huduma hiyo kwa umbali mrefu. 

Hata hivyo Waziri Mbarawa ameigiza pia DAWASA kuweka mitandao wa Maji safi kwa Maeneo yote yasiyokuwa na mitandao kabisa ili tenki hilo la Maji safi likikamilika liweze kunufaisha wakazi wote wa eneo la Saranga.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Prof Makame Mbarawa akionesha jambo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ( wapili Kulia)  wakati alipotembelea maeneo la Saranga na Kimara Temboni na kuagiza kujengwa kwa Tenki la Maji litakalohudumia eneo hilo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wakati alipotembelea  maeneo ya Saranga na Kimara Temboni.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akielezea jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa wakati alipotembelea maeneo la Saranga na Kimara Temboni na kuagiza kujengwa kwa Tenki la Maji litakalohudumia eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad