HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 3, 2018

BANC ABC YAWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA WANANCHI

Meneja wa Banc ABC tawi la Arusha, Magabe Nyambuche akizungumza jijini Arusha leo.

Na Mwandishi wetu, Arusha.

Banc ABC nchini imeendelea na juhudi za kuwekeza kwenye maendeleo ya jamii kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali, kusaidia jamii kupata bima za afya ili kuharakisha maendeleo ya jamii nchini Tanzania. Akizungumza jijini Arusha leo Meneja wa Banc ABC tawi la Arusha, Magabe Nyambuche amesema kwa mwaka huu 2019 wamejipanga kutoa mikopo kwa vikundi maalum vikiwemo vikoba na Saccos.

Vikundi mbalimbali vimekuwa vikipewa mafunzo na maafisa ustawi wa jamii ili waweze kunufaika na mikopo kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujinyanyua kiuchumi na taifa kwa ujumla. Nyambuche amesema Banc ABC imekuwa karibu na jamii hata kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali kupitia ubunifu wa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao na kuiwezesha benki hiyo kutwaa tuzo ya Ubunifu.

“Tunamawakala 250 ambao wanahakikisha kuwa wateja wetu wanafikiwa na huduma za kifedha popote pale walipo,” alisema Nyambuche.

Banc ABC imedhamini mkutano mkuu wa wadau wamaendeleo yajamii jijini Arusha ikiwa ni juhudi mojawapo ya kusaidia jamii ambayo hunufaika na utaalamu wa Maafisa wa Maendeleo katika maeneo ya vijiji na mijini.

Pia, Banc ABC imejizatiti katika kuendelea kushirikiana na serikali kuharakisha maendeleo ya jamii kwa kutumia dhana ya uwezeshaji wamikopo yenye masharti nafuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad