HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 9 December 2018

Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mtumishi wa afya

Mtumishi wa Wizara ya Afya kitengo cha maabara na mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma Mbwana Saidi Mbela , ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tigo Jigiftishe na kukabidhiwa zawadi yake jijini Da es Salaam.

Mbela anakuwa ni mshindi wa tatu wa zawadi ya shilingi milioni 10 ambayo hutolewa kila wiki kwa mshindi mmoja kupitia Promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe. Milioni 10 ya kwanza ilichukuliwa na David Mmuni huku ya pili ikienda kwa Iyaka Seifu Muinga.

Mbela aliungana na washindi wengine wanne ambao ni washindi wa kila siku ambao walikabidhiwa shilingi milioni moja moja .Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyika eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam, Mbela alisema alipigiwa simu kuwa ameshinda akiwa likizo jijini Dar es Salaam ambapo alikuja kumtembela shangazi yake.

“Niliamua kutumia likizo yangu kuja jijini Dar es Salaam kumsalimia shangazi yangu. Nilipofika tu nyumbani kwake Chamazi, nikapigiwa simu ya kuambiwa kuwa nimekuwa mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10,” anasema. Mbela aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusema kuwa atatumia fedha hizo kumalizia nyumba yake.

“Nawashauri watu watumie huduma za Tigo ili waweze kushinda. N rahisi sana kushinda haya mamilioni, mimi nimefanikiwa kushinda baada ya kuwa natumia huduma za tigo kama kutuma pesa, kununua muda wa maongezi, kununua umeme,” alisema .Akiongea wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yake, Shadya Bakari kutoka Tigo aliwataka wateja kuendelea kutumia huduma mbali mbali za Tigo ili kujishindia mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya kuwazawadia katika msimu huu wa sikukuu

Promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya. Promosheni itaongeza idadi ya mamilionea katika msimu huu wa sikukuu kwa kutoa zawadi kumi za shilingi milioni moja kila siku, zawadi moja ya shilingi milioni kumi kila wiki na zawadi kwa washindi wa jumla za shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50 itakayotolewa mwisho wa promosheni. 
 Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa kwanza kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Shadya Bakari (kulia) wa Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo
 Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa tatu kulia) akipongezwa na washindi wa kila siku wa shilingi milioni moja moja pamoja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika halfa iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam 
 Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Theresia Philipo (wa kwanza kulia) akilia kwa furaha wakati akikadihiwa  mfano wa yenye thamani ya shilingi milioni moja na Shadya Bakari (wa kwanza kushoto) kutoka Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo
 Washindi wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja moja katika Promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo wakiwa na nyuso za furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam

 Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja katika promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo, Hanifa Hassani Rashidi (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa wanyakazi wa Tigo Shadya Bakari (kusho) na Verykeys Julius katika haflaya kuwakabidhi washindi zawadi  iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam
Mmoja ya washindi wa kila siku wa shililingi milioni moja katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Khaled Miraji Sabuni (katikati) akipokea mfano wa hundi kwa wafanyakazi wa Tigo, Shadya Bakari (kushoto) na Verykeys Julius (kulia) katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam

 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad