HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 10 December 2018

RITA YAIBUKA MSHINDI KWA WAKALA WA BORA WA SERIKALI KWA KUANDAA NA KUWASILISHA TAARIFA ZA FEDHA ZENYE KIWANGO

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) imekabidhiwa tuzo kwa kuwa Taasisi katika kundi la Wakala bora ya Serikali ulioandaa na kuwasilisha taarifa za kifedha zenye kiwango cha Kitaifa na Kimataifa kwa mwaka 2017.

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt Ashantu Kijaji  mwishoni mwa wiki Desemba 8, 2018 katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akihutubia na kufunga mkutano wa mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu NBAA, amezitaka taasisi nyingine za Serikali kuiga mifano hiyo kwani awamu hii ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli inahimiza matumizi sahihi ya fedha za umma ili zitumike katika utoaji wa huduma bora sambamba na kulifikisha Taifa katika uchumi wa Kati wa kilimo na viwanda. 

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson amesema kuwa kwa tuzo waliopata inawapa moyo katika kuendelea kuchapa kazi kwa katika kuandaa vitabu vya mahesabu kwa viwango vya kitaifa na Kimataifa.

Amesema kuwa ushindi huo ni kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano na wahasibu na ndio matokeo yake taasisi inaibuka na ushindi ambao kila mtu anafurahi.Hudson amesema kuwa hata mwakani watafanya vizuri zaidi kutokana na ushindi huo ambao watu wengine wanakosa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhi tuzo kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson kwa Taasisi yake kuwa Wakala ya Serikali iliyoandaa taarifa bora ya kifedha yenye kiwango cha Kitaifa na Kimataifa kwa mwaka 2017, sherehe za makabidhiano ya tuzo hizo yaliyofanyika katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson akionesha tuzo ya kuwa uwa Wakala ya Serikali iliyoandaa taarifa bora ya kifedha yenye kiwango cha Kitaifa na Kimataifa kwa mwaka 2017, sherehe za makabidhiano ya tuzo hizo yaliyofanyika katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam. 
Picha ya pamoja ya wadau waliotunukiwa tuzo katika zinazotolewa na NBAA zilizofanyika katika katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad