HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 6, 2018

TADB ‘yatupa’ jembe la mkono kwa kuwakopesha matrekta wakulima wa pamba

Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imetoa matrekta 24 yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Masoko (AMCOS) 24 vinavyolima zao la pamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuongeza tija na uzalishajji wa zao hilo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo inalenga katika kuwawezesha wakulima wa zao la pamba nchini ili waweze kuongeza tija na uzalishaji kama inavyobainishwa katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Bw. Marco Mtunga amesema kuwa kupitia mkopo wa viua dudu uliotolewa msimu uliopita na TADB, ambapo uliwanufaisha zaidi ya wakulima laki sita wa zao la pamba ambapo uliwezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 221,600 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67 ikilinganishwa na tani 133,000 zilizozalishwa msimu wa 2017/18.

Bw. Mtunga ametoa wito kwa taasisi nyingine kushirikiana ili kuweza kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba hapa nchini.

Wakizungumza wakati wa makabdihiano hayo, baadhi ya wakulima walionufaika na matrekta hayo, waliishukuru serikali kupitia benki ya maendeleo ya kilimo kwa kuweza kuwakopesha matrekta hayo hali itakayochagiza tija na uzalishaji wa zao la pamba nchini.
 Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba (aliyevaa tai) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) wakikata utepe wakati wa kukabidhi matrekta 24 yaliyotolewa kwa vyama vya Ushirika vya Msingi na Masoko (AMCOS) za mikoa ya Kanda ya Ziwa. Matrekta hayo yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akikabidhi ufunguo wa trekta kwa mmoja kati ya viongozi 24 wa vyama vya Ushirika vya Msingi na Masoko (AMCOS) za mikoa ya Kanda ya Ziwa waliokopeshwa matrekta yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Wanaoshuhudia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine na baadhi ya viongozi wa AMCOS hizo.
 Pichani ni matrekta yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo kama mkopo kwa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko (AMCOS) 24 zinazolima pamba Kanda ya Ziwa. Mkopo huu umewezesha AMCOS hizo ‘kutupa‘ majembe ya mkono katika kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad