HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 6 November 2018

STARTIMES NA SOS CHILDREN’S VILLAGES ZAINGIA UBIA WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA VIJANA KWENYE AJIRA

\
 KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd na SOS Children’s Villages Tanzania wameingia  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi, lengo likiwa ni kuwapatia fursa  mbalimbali hasa kiteknolojia ili kuendana na malengo ya milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Katika mkataba huo StarTimes itasaidia programu mbalimbali za SOS Children’s Village katika Mikoa zaidi ya saba ikiwemo Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Iringa na Mufindi na program hizo zitalenga hasa kwenye kupanua nafasi za kujifunza na kukuza uzoefu miongoni mwa Vijana wa SOS Children’s Village. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo mwanasheria mkuu wa Star Media (T) Ltd Justine Ndege amesema  kuwa kwa vijana waliopo, kazi yao ya kwanza sio kuwa na uhuru. Kwao jambo la msingi kwanza ni kuishi tofauti ya maisha huru yenye heshima na maisha yenye misukosuko na mahangaiko ndicho wanacholenga kukabiliana nacho.

Ndege amesema kuwa, Ushirikiano baina ya kampuni Startimes na  SOS Village utapiga hatua katika kuwapeleka Vijana katika soko la ajira na kuwapatia namna au njia za kujitengenezea kesho yenye uimara na uhakika zaidi katika jamii zao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi mkuu wa SOS Childre’s Village Dvid Mulongo amesema kuwa moja ya mambo ambao StarTimes itafanya ni kuwapatia nafasi vijana kutoka SOS Villages Tanzania bara na Zanzibar kujifunza kwa vitendo kazi mbalimbali zilizopo kwenye kampuni yao, ushauri, mafunzo ya kiufundi kuhusu namna ambavyo StarTimes inafanya kazi hasa katika Idara ya Masoko na kuhusu bidhaa zake ili kukuza uelewa wa kazi na ajira kwa Vijana.

Mulongo amesema kuwa kampuni ya Star Media (T) Ltd itatumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuzungumzia juu ya programu za SOS Village ikiwa ni moja ya mambo ambayo yatafanywa chini ya ushirikiano huo ambao ni nafasi ya kipekee kwa Vijana kukua na kuendeleza kiuchumi.

Barani Afrika, watu milioni 200 wana umri kati ya miaka 15 na 24 ikiwa ni zaidi ya asilimia 20 ya watu wote kwa bara zima. Idadi inazidi kuongezeka kwa kasi, na itaongeza presha katika upatikanaji wa nafasi za kazi. Katika hii, Vijana ni 37% ya watu wanaofanya kazi, lakini bado Vijana ni 60% ya watu wasio na ajira. Nchini Tanzania kwa watu wanaoweza kufanya kazi (miaka 15 - 64) ni 23,466,616 ambayo ni sawa na 52.2% ya watu wote; Vijana (miaka 15 – 35) ni 15,587,621 sawa na 66.4% ya watu wanaoweza kufanya kazi.

Kwa ushirikiano huo wa StarTimes na SOS Children’s Village utasaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza Vijana ambao wataweza kuingia katika soko la ajira ili kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ukosefu wa ajira.
Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kuingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo
 Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto)  wakisaini  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
 Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto)  wakipeana mikono mara baada ya kumaliza kuingia  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad