
Akizungumzia
usajili unaoendelea katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo, Dokta
Chihoma amesema watu wengi wameitikia wito na wamejitokeza kwa wingi wao
kujiandikisha tayari kwaajili ya kushriki mbio hizo ambazo zilianzishwa
rasmi mwaka 2017 kwa malengo mengi lakini kubwa likiwa ni kuchangisha
fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo
imefanikia kuanza kwa kiasi kikubwa.
Aidha Chihoma ameongeza kuwa nafasi bado zipo wazi kwaajili washiriki watakaojitokeza kujiandika kwaajili ya bio hizo.
Kwa
upande wao wadhamini wa na waandaaji wa mbio hizo Mantra Tanzania au
Uranium one wamesema kila kitu kipo sawasawa na kuwataka watanzania na
wageni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo zinalenga
kuleta maendeleo ya kiafya katika eneo la Namtumbo na vitongoji vyake.
Mwakilishi
wa Mantra Tanzania Bi. Khadija Pallangyo Kawawa amaesema maandalizi
yanaendelea vizuri na kwamba watanzania watafurahia mbio za mwaka huu
kutokana na jinsi zilivyopata hamasa kubwa katika maeneo mbalimbali
“Nawaomba sana watanzania wajitokeze kwa wingi waje washiriki nasi
katika kufanikisha awamu ya pili ya Namtumbo Marathon”
Alisema
Khadija huku akiwaomba wana Namtumbo, Songea Ruvuma na vitongoji vyake
hasa wafanya biashara na wenye makampuni katika maeneo mbalimbali nchini
kujitokeza kwa wingi kuuchangia ujenzi wa hospitali ya wila ya Namtumbo
akiitaja hospitali hiyo kuwa itakuwa msaada mkubwa wenye kuleta
mafanikio na maendeleo katika eneo lote linalopakana na wilaya hiyo.
Nao
waratibu na wasimamizi wa tukio zima Corporate Info Limited ya jiji Dar
Es Salaam wamesema mbio hizo zinaandandaliwa kuja kuwa moja kati yam
bio kubwa kabisa nchini huku wakijivunia kuwa wasimamizi wa mbio hizo
kwa mara nyingine.
Wilaya
ya Namtumbo imezungukwa na vivutio mbalimbali vya kiasili mojawapo
ikiwa mbuga kubwa ya wanya ya Sloue ambayo imekuwa kivutio kikubwa sana
kwa watalii kutoka mataifa mbalimbali na ndani nchi hivyo kufanyika kwa
mbio hizo itakuwa sehemu mojawapo ya kuitangaza mbuga hiyo pamoja na
vursa zingine kama madini aina ya Uranium ambayo yanapatikana kwa wingi
wilaya Namtumbo.
No comments:
Post a Comment