HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 5 November 2018

CDF YATOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO KUPITIA MICHEZO.

Na Agness Francis, blogu ya Jamii. 


Taasisi inayopinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake CDF ikishirikiana na ISDI wamefanya bonanza kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu ya utokomezaji wa ukatili.

Boanza hilo lilofanyika katika  kata ya Kitunda halmashauri ya Ilala imehusha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu na kuhamasisha wanaume wawe mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia.


Akizungumza na waandishi wa habari Mgeni rasmi wakati wa bonanza hilo, Afisa Ustawi wa Jamii Ilala Joyce Maketa  amesema Kuwa kwa kuwakutanisha vijana katika bonanza hilo linasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii nzima katika kuhakijisha janga la ukatili wa kijinsia  linapingwa vikali hapa nchini. 


"Katika Kata ya Kitunda yapo mambo mbalimbali yanayohusisha ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto na kumpelekea kupoteza haki zake, na sana yanakuwa kwenye upande wa  kulawitiwa na ukeketaji, hivyo basi uwepo wa bonanza hilo litasaidia ongezeko la wigo la watu kupata ujumbe huo na ukatili wa kijinsia katika manispaa ya Ilala"amesema Maketa. 

Aidha Afisa Uhamasishaji wa wanaume jukwaa la utu wa mtoto CDF, Kiswigo Mwang'onda amesema Kuwa lengo la kuwepo kwa bonanza hilo na kushirikisha michezo ni kusaidia ukatili huo unatokomezwa kwa kuwa wanaume ndio vyanzo vya ukatili huo,kwa kuhakikisha mtoto anapata haki Zote zinazostahili kama elimu na mali.

"Baadhi ya wanawake wengine hapa nchini hufanya vitu ili waonekane bora kwa wanaume zao Kama suala la ukeketaji, ikiwa pia wanaume ndio sehemu ya matatizo hayo,kupitia michezo mwanaume atapata elimu ili kutatua tatizo hili na kuwa suluhisho la kudumu"amesema Mwang'onda. 

Hata hivyo Nahodha wa timu ya Kitunda, Miraji Suleiman amesema kuwa bonanza hilo Kwa ajili ya kupinga unyanyasaji,ukeketaji,ulawiti pamoja na mimba za utotoni litasaidia kutoa ujumbe kwa Jamii nzima ya wakazi wa kitunda."Taasisi kama hizi zikiwa nyingi na kuhamasisha upingaji wa ukatili kwa kutumia michezo kuna watoto pia watajifunza siku nyingine watakuwa wajumbe wazuri kuhusiana na ukatili kijinsia itasaidia jamii mbali mbali kupata elimu hiyo"amesema Nahodha Suleiman.

Afisa uhamasishaji wanaume na utu wa mtoto kutoka Taasisi ya  CDF Kiswigo Mwang'onda akizungumzia  lengo la kufanya bonanza hilo katika viwanja vya Shule ya Msingi Kitunda Jijini Dar es Salaam na kuhusisha vijana na kusaidia kutoa elimu Kwa wanaume juu ya utokomezaji wa ukatili kwa watoto na kinamama
Afisa Ustawi wa Jamii  Halmashauli ya Wilaya ya Ilala ambaye ni  Mgeni rasmi katika bonanza  kuhamasisha na kutoa elimu ya utokomezaji wa ukatili Joyce Maketa akisalimina na wachezaji wa mpira kabla ya kuanza kwa mechi katika Viwanja vya Shule  ya Msingi Kitunda Jijini Dar es Salaam.
Afisa Ustawi wa Jamii  Halmashauli ya Wilaya ya Ilala Joyce Maketa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa mpira pamoja na wafanyakazi wa  Taasisi za CDF na ISDI katika bonanza la kuhamasisha utokomezaji wa ukatili wa watoto na wanawake katika viwanja vya Shule ya Msingi Kitunda Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad