HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 23 November 2018

REA AWAMU YA III MZUNGUKO WA PILI KUNUFAISHA VIJIJI VILIVYOSALIA KUANZIA JUNE 2019

Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze

MWELEKEO wa mradi wa wakala wa umeme vijiji (REA III )mzunguko wa pili unatarajia kuanza June 2019 ,ili kuvifikia vijiji ambavyo vimesalia katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya kwanza.
 Aidha mradi wa ujazilizi unatarajiwa kuanza mwezi machi mwakani huku mradi wa peri -urban utakaohusisha mkoa wa Pwani na Dar es salaam unategemewa kupata mkandarasi Januari mwaka huo na umeshatengewa sh.bilioni 83.

Naibu waziri wa nishati, Subira Mgalu alieleza hayo katika kikao cha madiwani cha kata kwa kata kilichofanyika Lugoba Chalinze, mkoani Pwani ,wakati akitolea ufafanuzi utekelezaji unavyoendelea wa miradi ya umeme vijijini na mipango ya miradi hiyo ya kimkakati .

Alisema, kwa jitihada zote hizo za serikali kutekeleza miradi ya vijijini tayari vijiji 4,702 vimeshafikiwa hadi sasa . Subira alisema maeneo yote iliyolengwa wakandarasi wanaendelea na kazi. Kwa mujibu wake ,mkoa wa Pwani katika REA awamu ya III vipo vijiji 150 ,ambapo baadhi ya vijiji vimeshawekwa miundombinu na vingine mita .

Alilielekeza shirika la umeme (TANESCO) kuendelea kusambaza umeme kwenye maeneo ya wananchi pasipo kusubiri utekelezaji wa mradi wa REA. "Serikali inafanya kazi ,nia yetu ni ushindi na sio ushindi tuu katika chaguzi zinazokuja bali tuwe na majibu ya namna tunavyotekeleza ilani vijijini na vitongojini" alisisitiza Subira.

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ,Saidi Zikatimu aliiomba serikali kuwa, vijiji vinavyopitiwa na umeme vifikie vitongoji vyake na kufikia vijiji ambavyo tangu dunia iumbwe havina umeme. Diwani wa kata ya Miono ,Juma Mpwimbwi alieleza bado kuna tatizo la ukosefu wa umeme kijiji cha Mkwajuni na Makaomakuu ambapo tangu wapimiwe nguzo hawajapelekewa vifaa wala kuandaa miundombinu .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad