HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 6 November 2018

KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU

     Kaimu Katibu Msaidizi wa timu ya mpira wa miguu Manispaa ya Kinondoni (KMC) Walter Harrison akizungumza na wadau pamoja na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu kufukuzwa kwa mchezaji wao  Abdulhalim humud


Na.Khadija Seif,Globu ya jamii

Uongozi wa Klabu ya Kinondoni municipal council (KMC) Iimeweka wazi msimamo wao wa kumfukuza rasmi aliyekua mchezaji wa mpira wa miguu Abdulhalim humud.

Kaimu Katibu Msaidizi wa timu hiyo Walter Harrison amesema mchezaji huyo amefukuzwa rasmi kutokana na utovu wa nidhamu kwa viongozi wake pamoja na wachezaji wenzake.

Harrison ameeleza kuwa, vitendo vya Humud vya utovu wa nidhamu vimekua vikijirudia mara kwa mara na kwa uongozi kushindwa kuweza kuvikabili na kulazimika kumfukuza rasmi.

"Vitendo vya utovu wa nidhamu vimekuwa vinajirudia mara kwa mara, kwa viongozi na hata wachezaji wenzake na imepelekea kushindwa kuvumulia na kulazimika kuachana nae rasmi,"amesema Harrison


Alikadhalika Humud alishawahi kuandika barua kwa uongozi wa KMC kuomba kuachwa ili asiendelee kuichezea timu hiyo kwa sasa na hivyo uongozi wakaamua alipe gharama kiasi kutokana na pesa nyingi zilitumika kama vile gharama za matibabu, mshahara pamoja na fedha zilizokua zikitumika wakati yuko kambini.

Aidha , Kaimu Katibu huyo amekumbusha wadau na wanamichezo kuwa tabia hiyo kwa Humud imekua kama ni desturi yake kwani alishawahi kufanya vitendo hivyo kwa baadhi ya timu kongwe hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad