HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 6 November 2018

BENKI YA I & M IMETOA ZAWADI NONO KWA WATEJA WAKE 5 KATIKA KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU.

Na Agness Francis,Globu ya Jamii. 

Benki ya I & M imetoa zawadi nono kwa wateja wake katika droo  ya kwanza ya JIDABO na I & M bank chini ya usimazi kutoka bodi ya Taifa  ya michezo ya kubahatisha iliyochezeshwa leo ambapo washindi  watano wamepatikana kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini .

Droo hiyo imekuwa ni kwa wateja wao katika kuelekea msimu wa sikukuu ya Christmas na mwaka mpya  2018.

Akizungumza na waandishi wa  habari leo Jijini Dar es  Salaam  Mkuu wa kitengo cha Wateja na reja reja Ndabu Swere I & M benki amesema kuwa  promosheni hiyo iliyoanza mwezi Octaba na kuendelea mpaka Disemba kwa kila mwezi kutaja washindi watano wa droo hiyo.

"Washindi watano waliopatikana Leo ni sehemu ya wshindi 15 ambao watapatikana katika kipindi chote cha miezi  mitatu ya  JIDABO na I &M  ambayo ili kushiriki unapaswa kufungua akaunti  ya  akiba, akaunti ya mshahara au ya mtoto katika tawi lolote la benki yetu"amesema Swere. 

Aidha Swere ameongezea kuwa kwa mteja ambaye tayari  ana akaunti tayari ya benki hiyo anapaswa kuhakikisha kuwa ana akiba ya shilingi 200,000 ikiwa anashiriki akaunti ya biashara au 100,000 ikiwa anamiliki akaunti yingine  zinazohusika katika promosheni hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Uendeshaji   I & M Benki Donald Mate amewataja washindi wa promsheni hiyo ambao ni watano baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ambao ni  Selcom wireless LTD, Jumanne Mchench, Eliakunda Shoo,Sherbanu Osman, Eco dry Cleaners  LTD. 

Meneja Mauzo I & M benki  Norman Vasta  amebainisha kuwa kwa mujibu wa promosheni hiyo washindi hao watano  watapata mara mbili ya akiba zilizopo kwenye akaunti zao.

"kiwango cha juu zaidi  kutolewa kwa mteja kitkuwa shilingi 5,000,000,mfano ikiwa akiba ya mwezi husika ya mteja ni 5,000,000 basi atazawadiwa mara mbili na Kuwa 10,000,000"amesema Vasta.

Swere amemalizia kwa kuwataka watanzania wawe na utanaduni wa kuhifadhi akiba kwenye mabenki na kuchangamkia fursa hiyo ya kufungu akaunti katika Matawi yanayopatikana Mwanza,Kilimanjaro, Arusha pamoja na Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Reja Reja  Ndabu Swere I & M Benki akitoa wito na kuwataka watanzania wawe na utanaduni wa kuhifadhi akiba kwenye mabenki na kuchangamkia fursa hiyo ya kufungu akaunti katika Matawi yanayopatikana Mwanza,Kilimanjaro, Arusha pamoja na Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji I & M Benki Donald Mate  akiwataja washindi watano wa droo hiyo ya kwanza ya promosheni ya JIDABO na  I & M Benki iliyofanyika leo Jijini Dar es Salam.

Meneja Mauzo I & M Benki Norman  Vasta  akichezesha droo ya promosheni ya JIDABO na I & M Benki iliyofanyika leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam na kushoto ni mteja wa Benki hiyo akichagua karatasi ya mmoja ya  mshindi kati ya watano walioshinda  droo ya kwanza ya promosheni hiyo iliyosimamiwa na Chiku Saleh kutoka bodi ya  Taifa ya michezo ya kubahatisha.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad