HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 26 November 2018

iStore Tanzania yazindua simu mpya hapa nchini

DUKA la istore nchini Tanzania imezindua simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max inayoanza kutumia nchini kuanzia sasa. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtaalamu wa Bidhaa za simu za Apple, Salum Abdalla amesema kila nchi yao wana muda wa kuzindua simu mpya na kwa Novemba 23 imekuwa ni muda wa nchi ya Tanzania kuzindua simu ya iPhone Xs na iPhone Xs max.

Amesema wamezindua simu hiyo baada ya kukamilisha taratibi zote ikiwemo kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) ili kuitambulisha kwao na kuiruhusu kutumia mitandao ya hapa nchini. Abdalla amesema kila nchi ina taratibu zake na kwa Tanzania lazima wafike TCRA na iStore Tanzania imefanya jambo hilo na kwa hiyo sasa hivi
iPhone Xs na iPhone Xs max rasmi zinaweza kutumika nchini.

Akielezea utofauti wa simu ya
iPhone Xs na iPhone Xs max, amesema ni simu zenye uwezo mkubwa sana tofauti na simu zingine.
Mkurugenzi wa iStore Tanzania, Vipul Shah akizungumza na wanafamilia wa iStore Tanzania waliofika kwenye uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika dula la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa iStore Tanzania wakifuatila wakati wa uzinduzi wa Simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika dula la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa iStore Tanzania, Shamim Goliama(kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu simu mpya ya iPhone Xs na iphone Xs max kwa baadhi ya wateja waliofika kwenye uzinfuzi wa wakati wa uzinduzi uliofanyika katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakiangalia bidhaa za iStore wakati wa uzinguzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika dula la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa iStore Tanzania, Pareshi Gohil akitoa ufafanuzi kuhusu laptop kwa mmoja wa wateja waliofika kwenye uzinfuzi wa wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa iStore Tanzania, Vipul Shah(kushoto) akizungumza na mmoja wa wateja waliofika katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max.
Baadhi ya wafanyakazi wa iStore Tanzania wakitoa huduma mara baada ya kuzindua simu ya iPhone Xs na iPhone Xs max hapa nchini
Afisa masoko na Mtaalamu wa Bidhaa wa iStore Tanzania, Salum Abdalla akizungumza na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max ilinayoanza kutumika hapa nchini
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba Elias 'Barnaba'akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max iliyozinduliwa nchini Tanzania katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad