HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 26 November 2018

UPELELEZI KESI YA UCHOCHEZI INAYOMKABILI ZITO KABWE WAKAMILIKA

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi katika kesi ya uchochezi inayomkabili, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe umekamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi ameeleza hayo leo Novemba 26.2018 wakati kesi hiyo ilipokuwa kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.

Kufuatia kukamilika kwa upelelezi huo maelezo ya awali (PH) dhidi kesi hiyo ya Zitto yatasomwa Desemba 13,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi

Katika kesi hiyo Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi ya chama cha ACT Wazalendo, kwa nia ya kuleta chuki kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la polisi alitoa Maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Pia Zitto anadaiwa kutoa Maneno ya uchochezi ambayo yalikuwa na lengo lenye kuleta hofu.

Aidha Zitto anadaiwa Kutoa walaka kwa umma ukiwa na Maneno ya kichochezi kwa nia ya kuleta chuki kwa watanzania dhidi ya polisi.
 Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe  (wa pili kulia) akizungumza jambo na baadhi ya wadau wake/wanachama wa chama chake alipokuwa akitoka nje ya jengo la Mahakama ya Kisutu leo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad