HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 29 October 2018

WAKAAZI WA MWANZA WAPATA VIBE LA TIGO FIESTA

Kundi la Weusi lilkipagawasha mashabiki kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza usiku wa kuamkia jana. 

Wakaazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake usiku wa kuamkia jana waliweza kukonga mioyo yao kwa burudani kabambe kwenye Tamasha kubwa nchini la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba. Wasanii mbalimbali wakiwemo Weusi, Rostam, Country Boy, Nandy, Fid Q, Richie Mavoko, Jux,WhoZu Nedy Music na wengine wengi waliweza kufanya kile mashabiki walikuwa wanatarajia.

Mwamba wa kanda ya Ziwa Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q aliwateka vilivyo wanamwanza hasa kwa wimbo wake FRESH, Fid Q ambaye ni mwenyeji wa Mwanza ilimbidi arudie wimbo huo pendwa mbele ya mashabiki. Vibe la Tigo Fiesta liliamshwa zaidi na kundi la Weusi lililowajumuisha Joh Makini, Nikki wa Pili , Lord Eyez na G Nako walioweza kukaa jukwaani kwa muda mrefu bila kuchosha mashabiki kwa nyimbo lukuki zikiwemo SWAGIRE,NiCome na kadhalika.

Nae Msanii anayeng’ara kwa sasa, WhoZu aliweza kuwakamata mashabiki kwa wimbo wake HUENDI MBINGUNI amabo ameupiga kwa mahadhi ya Reggae. Kwa upande wa kundi la Rostam linalowajumuisha Roma na Stamina kama kawaida yao wao ndio wanaofunga jukwaa, waliweza kufunga shoo kwa nyimbo zao nyingi.

Nao Wadhamini wa Tamasha hilo Kampuni ya Tigo, Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madata alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Madata alisema.

Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz

Tamasha hilo litaendelea jumapili hii kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad