HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 5 October 2018

MADAKTARI BINGWA WA MOYO, USINGI KUTOKA SAUDIA ARABIA WAAGWA JKCI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohamed Janabi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo walioshiriki tukio la kuagwa kwa madaktari Bingwa wa magonjwa ya moyo, usingizi, wauguzi na watalaam wa mashine za moyo kutoka Saudi Arabia wapatao 11 waliokuwa wakisaidia kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.

MADAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo, usingizi, wauguzi na watalaam wa mashine za moyo kutoka Saudi Arabia ambao waliokuwa wakisaidia kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam wameagwa rasmi.

Tukio la kuagwa kwa madaktari hao wapatao 11 limefanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ambapo madaktari wa taasisi hiyo wamewapongeza kwa ushirikiano waliounesha kipindi chote wakiwa hapo.

Akizungumzia madaktari hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janab amesema wamekuwa nao tangu Septemba 29 mwaka huu na sasa wamemaliza muda wao, hivyo wanarejea nchini kwao kuendelea na shughuli za utoaji huduma za matibabu ya moyo.

Profesa Janab amesema katika kundi hilo lenye madaktari 11 kulikuwa na madaktari bingwa wa moyo, madaktari bingwa wa usingizi, wauguzi na wataalam wa mashine za moyo.

Pia baadhi ya madaktari wa JKCI wametoa shukrani kwa madaktari hao na kubwa zaidi ni utaalam ambao wameupata kutoka kwao.

Madaktari wa JKCI wamesema pamoja na kwamba madaktari hao wanaondoka bado kile ambacho wamekipata kutoka kwao kitaendelea kuwa msaada katika kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa moyo na kuwaaga madaktari hao huenda lisiwe nano sahihi zaidi, hivyo wanawaambia milango ili iko wazi hivyo wanaweza kuja tena wakati wowote.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na Mshauri Mkuu wa magonjwa ya moyo kutoka Albalsam, Dk. Emad Bukhari amesema wamefurahia ushirikiano walioupata kutoka kwa madaktari wa kada mbalimbali wa JKCI.

Amesifu huduma za matibabu zinazotolewa kwenye taasisi hiyo ambayo ni moja kati taasisi yenye watalaamu wabobezi katika tiba ya magonjwa ya moyo huku akitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuanzisha taasisi hiyo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na Mshauri Mkuu wa magonjwa ya moyo kutoka kutoka Albalsam, Dk. Emad Bukhari akizungumza wakati akitoa shukrani kwa baadhi ya madaktari waliokuwepo ukumbini hapo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na Mshauri Mkuu wa magonjwa ya moyo kutoka kutoka Albalsam, Dk.Emad Bukhari akimkabidhi cheti mmoja wa Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Viviene Mlawi kwa niaba ya madaktari wengine. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohamed Janabi. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad