HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 9 August 2018

KIJIJI CHA CHIMBILA B KUSAMBAZIWA MAJI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. milioni 250 kwa ajili ya usambazaji wa huduma ya maji safi katika kijiji cha Chimbila ‘B’ kichopo kata ya Mnacho.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Agosti 9, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mnacho wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.

Waziri Mkuu amesemaSerikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji, ambapo itahakikisha wananchi wanapata huduma hiyo katika  umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Amesema mbali ya maji kusambazwa kwa wananchi, pia yatasambazwa kwenye taasisi zote za umma zikiwemo shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Mnacho na kuzungumza na wanafunzi, ambapo amesema Serikali inatarajia kujenga mabweni mawili katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kuishi shuleni na kupata fursa nzuri ya kujisomea.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wanafunzi wa kike shuleni hapo kuiomba Serikali iwajengee mabweni ili waweze kuishi shuleni na kupata muda mwingi wa kujisomea.

Wanafunzi hao wamemueleza Waziri Mkuu kwamba kitendo cha kuishi nyumba kinawakosesha muda wa kujisomea kwa sababu ya hupangiwa kazi nyingi wanapofika nyumbani, hivyo kukosa muda wa kujisomea.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo katika Kijiji cha Chimbila B, Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 9 2018
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua darasa la kompyuta katika Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018, kulia ni Kaimu Mkuu wa Shule Muhsin Ibrahim.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkuu wa Shule Muhsin Ibrahim, baada ya kukagua darasa la kompyuta katika Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa Agosti 9 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018.

 Wananchi wa Kata ya Mnacho wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Mnacho, Wilayani Ruangwa, Agosti 9, 2018. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chimbila B, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho, Agosti 9, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa kata ya Nandagala wakati akiwasili katika uwanja wa zahanati ya kijiji cha Nandagala kwa jailli ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Agosti 8.2018
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani humo, Agosti 8.2018


 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimshuhudia aliyekua Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018
 Aliyekua Mwenyekiti wa Kata ya Nandagala Jafari Omari (katikati), akikabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Agosti 8.2018


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Nandagala Wilayani Ruangwa,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad