HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 22 July 2018

Waziri Mbarawa awaasa DAWASA wasikae ofisi wawe wabunifu

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza baada ya bodi ya Wakurugenzi kuzinduliwa leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi na wajumbe wa bodi wakiwa katika picha ya pamoja.
 WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, ProfesaMakame Mbarawa, akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya DAWASA,katika uzinduzi wa bodihiyo, Dar es Salaam, leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, ProfesaMakame Mbarawa, akizungumza wageni waliofika wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya DAWASA pamoja na kuwapatia vitendea kazi kwa kila mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

*Awataka wasikae ofisi wawe wabunifu
*awaambia DAWASCO wasiridhike na mapato waongeze idadi ya watumiaji maji.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa amezindua bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka (DAWASA) iliyo chini ya Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Julai 07 mwaka huu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji amezindua bodi hiyo baada ya kukamilisha uteuzi wa wajumbe tisa wanaokamilisha Bodi ya DAWASA.

Akizungumza wakati wa kuzindua bodi hiyo, Prof Mbarawa amesema kuwa ana imani na bodi iliyoteuliwa kuwa itafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kuleta maslahi mapana kwa wananchi .

Prof Mbarawa amesema anahitaji taasisi kama DAWASA kuwa wabunifu na kuweza kufanikisha upatikanaji wa wateja wapya ili huduma za maji ziwafikie watu wote pamoja na kuongeza pato la nchi.

Amesema kuwa, bodi hii wanaamini watasimamia vizuri utendaji wa kazi wa mamlaka hizi kwakuwa kumekuwa na upotevu mkubwa wa maji na hilo linasababishwa na baadhi ya viwanda kuiba maji na kuitia hasara serikali.

" katika viwanda vya bia asilimia 75 ya uzalishaji maji ndiyo yanatumika ila kumekuwa na upotevu mkubwa  sana wa maji na pia kuna kiwanda sitakiweka wazi ambao kwa mwezi wanatumia lita Milioni 60 za maji ambazo ni Milioni 2 kwa siku lakini ukija katika malipo yao wanasema wanatumia Lita Milioni 17,"amesema Prof Mbarawa.

Ameeleza kuwa DAWASCO ambao ndiyo wasimamizi wa maji wamekuwa hawafanyi kazi zao inavyotakiwa kwa kutokuwafuata wateja kitu ambacho kinapunguza ufanisi wao wa kazi na kumtaka Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja kubadilika na kuacha kukaa ofisini bali anatakiwa awafuate wateja na kufahamu mahitaji yao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof Kitila Mkumbo amesema kuaa mahitaji ya maji katika jiji la Dar es Salaam ni makubwa sana na kumekuwa hakuna upigaji wa hatua kwenye suala la upatikanaji wa maji.

Amesema kuwa hilo linatokana na mamlaka husika za maji kuridhika na mapato wanayoyapata kila mwezi katika ukusanyaji wa ankara ila ila kwa upande wa serikali wamekuwa wana malengo mengine zaidi.

" Mamlaka husika zimekuwa zinaridhika na mapato wanayoyapata hususani kutoka kwenye viwanda kama TBL na SBL ila sisi kama serikali ni kuona idadi ya watuw wangapi wameunganishwa na huduma za maji safi,"amesema Prof Mkumbo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa atafuata agizo la waziri na hawataishia katika makaratasi na watapambana kuhakikisha wanaiweka DAWASA katika sura mpya, pia kazi hiyo siyo ndogo bali kuna mengi yanahitajika kufanywa.

Bodi ya DAWASA inaongozwa na Jenerali Mstaafu akisaidiwa na wajumbe Mhandisi Nadhifa Kemikimba, Edward Mhede, Spora Liana,Dkt Fred Msemwa, Zuber Samataba, Mhandisi Gaudence Aksante,Rosemary Kasongo na Latson Msongole.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad