HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 22, 2018

WAZIRI MBARAWA AIPONGEZA DAWASA KUONGEZA MAJI DAR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Mbarawa ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  (DAWASA) kwa jitihada kubwa wanayoifanya ya kujenga mitambo ya maji iliyoongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 300 hadi 502 kwa siku.

Prof Mbarawa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi wa DAWASA inayoongozwa na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.

Amesema anatambua wazi kuwa kazi ya ujenzi wa mitambo ni kazi ngumu na inahitaji weledi mkubwa kuikamilisha ila DAWASA wameweza kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa miundo mbinu hiyo kwa maslahi ya wananchi.

Prof Mbarawa amewataka DAWASA kuongeza juhudi na bidii katika kukamilisha kazi ya usambazaji maji kwa kuwasimamia wakandarasi kwa karibu.

Katika hatua nyingine Waziri Prof Mbarawa ameeleza kusikitishwa na wingi wa maji yanayopotea kila siku bila kujulikana sababu na kusema karibu nusu ya maji yanayozalishwa yanapotea hivihivi.

 "Nusu ya lita milioni 502 zinapotea kila siku, na maji hayo yangekuwa yanamwagika hapa Dar es salam kungekuwa ni ziwa kinachotokea ni kuwa maji mengi yanaibiwa na watu wasio waamifu," alisema huku akionesha wazi kukerwa . 

Akimaliza kutoa pongezi hizo kwa DAWASA, Prof Mbarawa amesema kuwa sasa anataka kuanza ukurasa mpya utakaolenga kuboresha huduma kwa wananchi ya serikali yaliyowekwa ya kumfikia kila mwananchi atumie maji safi na salama.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na watendaji kutoka Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (DAWASA) na kuwapongeza kwa juhudi wanazozifanya za kutekeleza na kusimamia miradi ya maji na kuweza kuongezeka kwa upatikanaji wa maji kufikia Lita Milioni 502 kwa siku.
 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (DAWASA) wakifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi wa bodi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Awesu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Dr Suphian Masasi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi na watendaji wengine wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka DAWASA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad