HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 26 July 2018

MBARAWA AAGIA DAWASCO KUWEKA MITA ZA PRE PAID KATIKA VIWANDA VYOTE JIJINI DAR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI  wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa amewaagiza Shirika la Maji safi na Maji taka (DAWASCO) kubadilisha mita zote za maji kwa viwanda vyote vya Dar es Salaam na wale wateja wakubwa.

Hayo ameyasema leo alipotembelea viwanda vya Azam Bakheresa, Pepsi na Coca Cola ili kuweza kuona kila mteja anapata maji kwa maslahi anayoyahitaji.

Prof Mbarawa amesema kuwa amewaagiza DAWASCO kufunga mita za malipo ya kabla  (Pre Paid) zitazomuwezesha mteja kununua maji kulingana na matumizi yake ambapo atahitaji kulipia kwanza kabla ya kupatiwa maji na hela itakapomalizika maji hayatatoka.

"Mfumo huu wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid) utamfanya mteja atumie maji kulingana na mahitaji yake na atalipia maji kabla na hela yake itakapoisha maji hayatatoka na hilo litasaidia kwa kila kufahamu matumizi yake sahihi ya maji,"amesema Prof Mbarawa.

Ameeleza kuwa, viwanda vyote na wateja wakubwa watafungiwa mita hizo ambazo zitakuwa zinaendeshwa kwa mfumo wa kidigitali na utasaidia kusimamia maji yanayostahili kutumika pia fedha wanazostahili kuzipata kutoka katika maji hayo.

Prof Mbarawa amesema , " Matumizi haya ya mita za malipo ya kabla  yataweza kusaidia kupunguza upotevu wa maji na watu hawataweza kuzichezea kwa lengo la kuiba maji kwani zitakuwa zinasimamiwa moja kwa moja na DAWASCO,"

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kulikua na changamoto kubwa ya madeni kwa wale wadaiwa wa muda mrefu ila watakapowafungia mita hizo za malipo ya kabla kila watakapokuja kununua maji watakatwa kiadi fulani cha fedha ili kufidia malimbikizo yao.

Luhemeja amesema, zoezi hilo la ufungaji wa mita hizo utaanza siku ya Jumatatu na utaanzia kwa Waziri mwenyewe na kisha kwenda katika viwanda vya TBL, Coca Cola, Pepsi na Azam Bakharesa Tazara.

"Kwa kufungwa kwa mita hizo kutasaidia sana kutambua bili sahihi ya maji mtu atakayokuwa anatumia, kutokubambikiwa madeni pamoja na malipo hewa,"amesema Luhemeja.

Wananchi mbalimbali wameonekana kufurahishwa na mfumo huo mpya utakaokuja na kusema kuwa utawasaidia mpaka wale wananchi wenye kipato kidogo kutumia maji kulingana na matumizi yao na wanaimani utasaidia sana taifa katika kuongeza pato lake.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa eneo la Mwenge akiwaelezea mfumo mpya wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid) utakaoanza kutumika hivi karibuni. Hayo aliyasema katika ziara yake katika Viwanda mbalimbami leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Maji taka (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid) baada ya kumaliza ziara ya kutembelea viwanda mbalimbali Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Kiwanda cha Soda Pepsi alipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kukagua mita za maji iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akikagua mita ya maji katika Kiwanda cha Pepsi leo Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad