HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 26, 2018

STARTIMES WAZIDI KUNOGESHA BURUDANI YA SOKA

Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes wametangaza kuonesha mechi za maandalizi ya Msimu mpya kwa ligi kubwa za barani Ulaya ambapo zitawashirika timu 18 bora kutoka ligi kubwa tano duniani.

Mechi hizo ambazo huchezwa chini ya mashindano yanayofahamika kama Kombe la Mabingwa wa Kimataifa( ICC) yatari zimeanza kutimua vumbi wikiendi iliyopita.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Startimes David Malisa amesema kuwa kama ulikuwa unajiuliza nini kinafuata baada ya Kombe la Dunia basi majibu ni hayo.

"Katika kuonyesha kwamba sisi ni wafalme wa Burudani, kutakuwa na mechi kali za ICC, maarufu kama Pre-Season yaani mechi za kujiandaa na msimu mpya.

"Ambapo utawaona wachezaji wakubwa kama Ronaldo akiwa na klabu yake mpya ya Juventus, Mahrez akiwa na Man City, Mo Salah, Mane, Messi na wennane wengi,"amefafanua .

Amesema kuwa mechi hizo za ICC ama Pre-Season zinapatikana kwenye king’amuzi cha StarTimes pekee hakuna king’amuzi kingine kinachoonesha.

 " Mechi zote zitaonekana kwenye chaneli ya World Football na Sports Premium ambazo zipo katika kifurushi cha MAMBO kwa watumaji wa Antenna Tsh 13,000 tu kwa mwezi na kifurushi cha SMART kwa wateja wa Dish kwa Tsh 19,000 kwa mwezi,"amesema.

Zamaradi Nzowa, Meneja wa kitengo cha Maudhui, StarTimes.“Katika kujali mahitaji ya wateja wetu pendwa kabisa, tumeongeza chaneli 5 mpya zaidi ambazo zitaanza kuonekana katika king’amuzi chetu kuanzia tarehe moja mwezi wa nane, chaneli hizo ni EBONY LIFE ya Nigeria, EWTN, Discovery Family ambayo ina vipindi vingi vya kifamilia, na DW kwa ajili ya Habari, pia tumeirudisha chaneli ya TV Imaan. Mbali na chaneli mpya tumeihamisha chaneli ya Fox Sports kutoka kifurushi cha UHURU kwenda kifurushi cha MAMBO

Miongoni mwa timu hizo ni Bayern Munich, Borussia Dortmund (Bundesliga), Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal (Premier League), PSG (League 1), Barcelona, Real Madrid (La Liga), AC Milan, Inter Milan na Juventus (Serie A). Katika mechi zilizopigwa wikiendi iliyopita Borussia Dortmund wameonyesha kiwango kizuri baada ya kuwafunga Manchester City 1-0 na kuwachapa Liverpool 3-1.

Wapenzi wa Soka nchini watapata nafasi ya kuishuhudia michuano hii kupitia chaneli ya World Football na Sports Premium katika king’amuzi cha StarTimes ambao wana haki za kipekee za kuonyesha michuano hiyo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuonyesha michuano ya ICC inayoendelea katika mabara matati tofauti ikizihusisha timu 18 bora kutoka ligi tano bora duniani. Kulia ni Meneja Maudhui wa Startimes Zamaradi Nzowa.

Meneja Masoko wa kampuni ya Startimes David Malisa akiwa pamoja na Meneja maudhui Zamaradi Nzowa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad